TAARIFA KWA UMMA KIKAO CHA WAZIRI WA KILIMO NA MAAFISA KILIMO WA MIKOA NA HALMASHAURI
Dodoma,
27 Januari 2021
Wizara
ya Kilimo imeandaa kikao kazi cha Waziri wa Kilimo na Maafisa Kilimo wa Mikoa
na Halmashauri nchini kwa lengo la kujadili changamoto za upatikanaji huduma za
ugani na nini kifanyike kuwasaidia wakulima kuboresha kilimo ili kiwe na tija.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb)
imesema kikao hicho kitajadili na kuweka mikakati ya utekelezaji wa kuhakikisha
wizara inaleta mapinduzi makubwa na kukifanya kilimo kuwa cha kisasa na chenye
faida kwa mkulima kwa kuzingatia Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu
ya Pili (ASDP II).
Mkutano huo utafanyika tarehe 29-30 Januari ,2021 katika ukumbi wa
Mikutano wa LAPF Jijini Dodoma kuanzia saa 3.00 asubuhi.Katika kikao hicho
Wizara itaelezea vipaumbele na mwelekeo wake katika kipindi cha miaka mitano
ijayo (2020-2025).
Imetolewa na;
Gerald M. Kusaya
KATIBU
MKUU
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...