Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu akizungumza na waandishi wa habari.
………………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu, Simanjiro
TAASISI ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa TAKUKURU Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara,
inamshikilia Mwenyekiti mstaafu wa Kijiji cha Kimotorok, Merubo Parimelo
na mjumbe mstaafu wa Serikali ya Kijiji hicho Daniel Melau.
Mkuu wa TAKUKURU
Mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu amesema watuhumiwa hao
wanashikiliwa kwa tuhuma za mbalimbali ikiwemo kughushi na kujipatia
fedha kwa njia ya udanganyifu.
Makungu amesema watuhumiwa hao walipopekuliwa wamekutwa na nyaraka za Serikali.
Amedai kuwa
watuhumiwa hao wamekuwa wakizitumia nyaraka kuuza ardhi ya kijiji kwa
kurudisha tarehe nyuma ili kuonyesha mauzo hayo yalifanyika wakingali
madarakani.
“Uchunguzi zaidi
umeonyesha kuwa baadhi ya wenyeviti wastaafu wa vijiji katika Wilaya ya
Simanjiro huondoka na nyaraka za vijiji kwa nia ya kutenda uhalifu wa
kuuza ardhi japo wameshaondoka madarakani,” amesema.
Amewataka wote walioondoka na nyaraka wazirejeshe mara moja na kuzikabidhi kwa maofisa watendaji wa vijiji wanaohusika.
“Wasiporejesha wafahamu kuwa watakutana na mkono wa sheria kama wenzao kina Parimelo na Melau,” amesema Makungu.
Amewataka wafahamu kuwa Serikali ina mkono mrefu hivyo itaendelea kuwafuatilia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...