IMEELEZWA kuwa, Bodi ya Ushauri ya Hospitali za Watu Binafsi (Private Hospitals Advisory Board- PHAB) ni chombo chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kilichopewa jukumu la kutoa ushauri katika usajili na usimamizi wa Huduma za Afya zinazotolewa na Vituo Binafsi, Taasisi za Dini, Kampuni na Asasi mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi imeelezwa kuwa bodi hii iliundwa kwa Sheria ya Bunge No.26 ya mwaka 1991. Kwa mujibu wa Sheria ya Uongozi wa Hospitali Binafsi ya mwaka 1977, (Private Hospitals (Regulation) Act, 1977) iliyofanyiwa marekebisho mwaka 1991.

Imeelezwa kuwa bodi hiyo inahusu uendeshaji wa Hospitali Binafsi hivyo, tumekaa na tayari wamefanya vikao kujadili mafanikio na changamoto   mbalimbali na Wajumbe wa Bodi wanapongeza sana sekta binafsi kwa kuisaidia serikali katika kuboresha huduma za afya nchini ambazo zimesogezwa karibu na wananchi.  Jumla ya vituo 2516 vimesajiliwa hapa nchini.

Imeelezwa kuwa pamoja na mafanikio  ambayo yamefikiwa katika serikali ya awamu ya tano, Bodi imebaini kuwepo kwa changamoto ya baadhi ya watumishi wa Umma kutumia muda wa Serikali kufanya kazi katika Hospitali Binafsi ambayo ni kinyume na kanuni namba 43 ya kanuni za Utumishi wa Umma ya mwaka 2003 (GN No. 168) na kanuni F. 3(1) (a) (b) na (c) za kudumu za Utumishi wa Umma za 2009. Kutokana na changamoto hiyo, serikali kupitia Bodi hii inaelekeza mambo mbalimbali ikiwa paamoja na:

Watumishi wote wa serikali wasitumie muda wa saa za kazi serikalini kufanya kazi katika vituo vya watu binafsi na hiyo ni pamoja na  Waganga Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Wafawidhi wa Vituo na Waratibu wafanye ufuatiliaji wa karibu kuhakikisha kuwa vituo hivi vinafuata sheria za Utumishi wa Umma na za Hospitali Binafsi

Pia Waganga Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wafawidhi wa Vituo waweke/wasimamie mifumo ya kuhakikisha watumishi wa Umma wanakuwepo katika vituo vyao ndani ya saa za kazi.  

Aidha imeelekezwa kuwa Wamiliki wa vituo binafsi wahakikishe watumishi wa Umma hawafanyi kazi kwenye vituo vyao katika muda wa serikali na yeyote atakayebainika amevunja sheria atachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo.

Vilevile imeelekezwa kuwa, Watumishi wa Umma wanaofanya kazi katika Hospitali binafsi wasitoke katika vituo vyao vya ajira wakati wa Muda wa kazi.  Mtumishi yeyote atakayethibitika kufanya hivyo atachukuliwa hatua kali pamoja na mmiliki wa kituo atakachokuwa akifanya kazi ndani ya muda wa kazi.  Hivyo, ni vyema wamiliki wa vituo hivi wahakikishe kuwa suala hili linazingatiwa. 

Aidha, wamiliki wa Hospitali Binafsi wahakikishe kuwa wanafuata Sheria, kanuni, miongozo na taratibu, za usajili wa vituo hivi ikiwemo watumishi wanaowasimamia.  

"Nawakumbusha wamiliki wote wa vituo binafsi nchi nzima kufanya kazi kwa kushirikiana na Bodi za usimamizi wa kutoa huduma za afya ili kuweza kuboresha huduma zetu kwa kufuata Sheria, kanuni, miongozo na taratibu zilizopo ili kutoa huduma bora kwa wananchi." Imeeleza taarifa hiyo.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...