Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza S.Johari akifungua rasmi awamu ya kwanza ya mafunzo ya ndege zisizo na rubani maarufu kama ndege nyuki(drone),mafunzo hayo yanatolewa na Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC)kinachomilikiwa na TCAA  kwa ushirikiano na chuo cha Pro Wings kutoka Afrika ya Kusini, yanafanyika kwa muda wa wiki nne(moja darasani , tatu mafunzo kwa vitendo.)


Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC)kinachomilikiwa na TCAA, Aristid Kanje akielezea muhtasari wa mafunzo hayo wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo ya wiki nne kuanzia Januari nne 2021.



Mkurugenzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Pro Wings kutoka nchini Afrika ya Kusini,Benjamin Mabeta akiwakaribisha washiriki na kueleza yale watakayojifunza katika muda huo wa wiki nne.



Washiriki wa mafunzo ya  awamu ya kwanza ya mafunzo ya ndege zisizo na rubani maarufu kama ndege nyuki(drone) wakifuatilia ufunguzi rasmi ya mafunzo hayo.mafunzo hayo yanatolewa na Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC)kinachomilikiwa na TCAA  kwa ushirikiano na chuo cha Pro Wings kutoka Afrika ya Kusini.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza S.Johari(aliyeshika ndege nyuki) akiwa kwenye picha ya pamoja na walimu na washiriki , baada ya kufungua  rasmi awamu ya kwanza ya mafunzo ya ndege zisizo na rubani maarufu kama ndege nyuki(drone),mafunzo hayo yanatolewa na Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC)kinachomilikiwa na TCAA  kwa ushirikiano na chuo cha Pro Wings kutoka Afrika ya Kusini, yanafanyika kwa muda wa wiki nne(moja darasani , tatu mafunzo kwa vitendo.)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...