Na Woinde Shizza ,ARUSHA
Mamlaka
ya mapato Tanzania (TRA) wafanya bonanza la michezo mbalimbali jijini
Arusha katika maadhimisho ya mapinduzi ya Zanzibar ili kupunguza msongo
wa mawazo ya ukusanyaji Kodi lakini pia kuwaleta kwa pamoja watumishi.
Akizungumza
wakati wakiendelea na michezo mbalimbali Kamishna mkuu wa TRA Edwin
Mhede amesema kuwa kazi zao zimekuwa na changamoto kubwa katika
ukusanyaji wa Kodi hivyo michezo itawasaidia kubadilishana
mawazo na kujadili mambo mbalimbali .
"
Michezo ni afya ,michezo ni undungu hivyo tukikutana tukajumuika kwa
pamoja katika sikukuu hii ya kitaifa ili tutakaporudi kazini tuwe na
afya njema "
Aidha
amesema kuwa kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni kuhamasisha
wafanyabiashara kutumia mashine ya EFD pamoja na wananchi kudai risiti
pindi wanaponunua bidhaa ili kuhakikisha wanapata bidhaa zenye uaminifu
.
Mhede amesema lengo la kufanya bonanza hilo katika mkoa wa Arusha
kwa sababu wako kwenye majadiliano ya mikakati ya nusu mwaka jijini humo .
Aidha
aliwaagiza kila viongozi wa TRA kila mkoa kuandaa simu ya bonanza
Katika mkoa wake na wasifanye Mara moja moja bali wawe wanafanya
mabonanza ya wafanyakazi wa mamlaka hiyo kila Mara kwani michezo
inaongeza ufanisi Katika utendaji kazi wao.
Bonanza
hilo limefanyika katika viwanja vya chuo cha uhasibu IAA wakijuhusisha
na michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, Pete ,vikapu kuruka kamba
pamoja na kufukuza kuku.
Naye
meneja utawala TRA Yasin Mwita ameeleza namna michezo itakavyo
wasaidia kuwa wakakamavu katika suhala zima la ukusanyaji Kodi kwani
wanafanyakazi kwa muda mrefu hivyo mazoezi Yana umuhimu kwao.
"
Tunakazi nyingi Sana ambazo zinatupelekea kuwa na changamoto hivyo
michezo hii ina umuhimu kwetu ili tuweze kukabiliana na changamoto
zilizopo katika kazi zetu"
Kwa
upande wake meneja wa TRA mkoa wa Songwe Farence Mniko amefurahia
maazimisho hayo yaliyofanyika kwa kutumia michezo mbalimbali kwani
wametengeneza mahusiano mazuri na wafanyakazi walioko mikoa mbalimbali
kwa kubadilishana ujuzi.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...