Na Said Mwishehe, Michuzi TV
BALOZI wa Ufaransa nchini Tanzania Frederick
Clavier amewakutanisha wasanii mbalimbali pamoja na wanafunzi zaidi ya 300
kutoka Vyuo Vikuu kupitia tamasha kubwa la buradani sambamba na mdahalo
uliokuwa unalenga kujadili na kubadilisha mawazo kuhusu njia sahihi za
kuendelea kudumisha upendo, umoja na mshikamano katika jamii.
Tamasha hilo limefanyika Januari 28,2021 katika
Kituo cha Utamaduni cha Alliance de France kilichopo jijini Dar es Salaam
kuanzia saa 12 jioni hadi saa tano usiku.
Balozi Clavier alipata nafasi ya kushuhudia kazi
mbalimbali za wasanii kuanzia za uchoraji, ngoma za asili na waimbaji wa muziki
wa dansi pamoja na sarakasi.Pia alipata nafasi ya kupiga kubadilishana na
mawazo na vijana mbalimbali waliohudhuria tamasha hilo.
Wakizungumza wakati wa tamasha hilo, wasanii
wamesema Serikali ya Ufaransa kupitia Ubalozi wake wa nchini Tanzania umefanya
jambo kubwa na nzuri la kuwakutanisha vijana katika kubadilishana mawazo kuhusu
njia sahihi za kudumisha umoja, upendo na mshikamano lakini wakati huo huo
wasanii wakipata nafasi ya kutoa burudani wakati taasha linaendelea.
Kwa upande wake Msanii maarufu katika muziki wa
kizazi kipya Ben Pol amesema kwamba wanatoa shukrani kwa Ubalozi wa Ufaransa
kwa kuonesha kujali na kuwathamini wasanii wa Tanzania kwa kuwapa nafasi ya
kuonesha uwezo wao katika tasnia ya sanaaa.
"Nimefurahi sana kupata nafasi ya kushiriki
katika tamasha hili la burudani, limeandaliwa kwa mpagilio mzuri, tumepata
burudani na wakati huo huo tumeshiriki katika mjadala wa kubadilisha mawazo
kuhusu namna nzuri ya kudumisha umoja wetu ndani ya jami bila kujali dini, rangi
wala kabila,"amesema Ben Pol.
Amesisitiza kuna kila sababu yakuhakikisha sekta
ya sanaaa inasimamiwa vema kwani imetoa mchango mkubwa katika kufanikisha
vijana kujiajiri na kuendesha maisha yao."Tuendelee kusapoti sanaa ya nyumbani,
tuendelee kuwainua na kuwapa nguvu wasanii, sanaa ni ajira na hivyo lazima
isimamiwe vyema kupata wasanii wengi ambao wajiajiri kupitia sana.
Kwa upande wake Rais wa Serikali ya Wanafunzi
kutoka Chuo Kikuu cha Elimu Dar es Salaam(DUCE) Said Masanga amesema wamejifunza
mambo mengi kupitia tamasha hilo na hasa wakati wa mdahalo ukiendelea na kubwa
zaidi ni jinsi gani ya kuishi katika jamii yenye watu wengi na mchanganyiko wa
tamaduni.
Ametumia nafasi hiyo kutoa mwito kwa wanafunzi na
vijana kwa ujumla kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri ya kujiajiri badala ya
kusubiri kuajiriwa kwani hivi sasa changamoto ya uhaba wa ajira ni
kubwa."Elimu ambayo tunaipata darasani iwe mwanga wa vijana kujiajiri
badala kusoma na kusubiri kuajiriwa.
"Tutumie elimu yetu kuipeleka kwenye jamii
ili kuleta maendeleo ya kila mmoja wetu, huo ndio mwito wangu kwa vijana na
hasa waliokuwa vyuo vikuu, tusisubiri kuajiriwa, tujiandae kujiajiri baada ya
kumaliza masomo."
Kuhusu tamasha hilo amesema watu wamechangia
katika maeneo mengi na kuuliza maswali na moja ya swali ambalo limeulizwa ni
jinsi wataweza kuishi katika tamaduni tofuati tofauti ndani ya jamii.
Hata hivyo Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na
Utamaduni katika Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania Cecile Frobert amesema
kuwa ubalozi huo unajisikia furaja kubwa kuona tamasha hilo limefanikiwa kwa
kiwango kikubwa na wasanii mbalimbali wakubwa wamehudhuria.Pia wanafunz zaidi
ya 300 kutoka Vyuo Vikuu wameshiriki mdahalo uliokuwa umeandaliwa wakati wa
tamasha hilo.
"Serikali ya Ufaransa kupitia Rais wetu Emmanuel
Macron moja ya mkakati wake ni kujenga upya uhusiano mzuri baina ya nchi yao na
nchi nyingine za Afrika ikiwemo Tanzania.Tunatambua nafasi ya sanaa na
utamaduni wa kila nchi na ni jukumu letu kuuendeleza kwa kuwawezesha wasanii
kuonesha vipaji vyao na kuibua wasanii wapya,"amesema Frobert.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...