Mbunge wa Mvemero Jonas Zeeland akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mvomero mkoani Morogoro.


Kikao Cha Baraza la Madiwani kikiendelea.


*Zeeland aahidi kuwachukulia hatua Watendaji hao

 Na Chalila Kibuda,Michuzi TV 

MBUNGE wa Mvomero Jonas Zeeland amesema wapo baadhi ya watendaji wanafanya uzembe wakutopeleka fedha za mfuko wa Jimbo kwenye miradi.

Akizungumza katika wa  Baraza la Madiwani  Halmashauri ya Mvomero , Zeeland amesema fedha za miradi  mpaka Sasa bado hazijafika na tayari zimeshazigawanywa kwa kata zote na kuahidi kuanzia sasa mtendaji yeyote atayezembea au kuzitumia fedha hizo kinyume na utaratibu atachukuliwa hatua za kinidhamu.

 "Ninaomba fedha ambazo tumezigawanya ziende sasa na mimi  Mbunge wenu   nataka twende kwa Kasi kubwa  kutekeleza miradi na kutatua changamoto za wananchi ikiwemo ukusanyaji wa mapato nao tuongeze nguvu"amesema Zeeland

Mbunge Zeeland amesema ameshafanya mawasiliano na Waziri wa Maliasili na Utalii amekubali kufanya kikao na uongozi wa Halmashauri ya Mvomero kwa ajili ya kutatua kero ya wanyama wakali tembo ambao wanapoteza maisha ya wananchi.

Amesema kikao hicho kitafanyika Februari wakati wowote tujiandae katika kutatua tatizo mara moja.

"Mimi ni mbunge wenu wa Jimbo hili la Mvomero kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Halmashauri na Mkurugenzi  tumeanza sasa kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali kutokana na  ziara ambazo nimefanya  maeneo mbalimbali ya Jimbo." amesema Zeeland.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...