Waziri
wa Nishati Dkr Medard Kaleman, akizungumza kwenye kituo cha kupokea
umeme,kusambaza na kupoza kilichopo eneo la Bulyanhuru wilayani Kahama,
kulia ni Mbunge wa Jimbo la Msalala Iddi Kasimu
Na Marco Maduhu -Kahama.
Waziri wa Nishati Dk. Medard
Kalemani, ameendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Shinyanga, ambapo
leo ametembelea Mgodi mdogo wa uchimbaji madini ya dhahabu Nyangalata
uliopo Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama.
Akiwa katika mgodi huo,
akiambatana na Mbunge wa Jimbo la Msalala Iddi Kasimu, Mkuu wa wilaya ya
Kahama Anamringi Macha, pamoja na maofisa kutoka Shirika la umeme
Tanzania (TANESCO), Dk. Kalemani amesema Serikali inataka kasi ya
usambazaji umeme kwenye migodi midogo ya madini ili kuondoa gharama
kubwa za uzalishaji wa madini hayo.
Amesema kwenye migodi midogo ya
uchimbaji wa madini ya dhahabu, hua wanatumia gharama kubwa ya
uzalishaji wa madini hayo kutokana na kutumia mafuta mazito ama
Jenereta, lakini wakitumia Nishati ya umeme kutoka Gridi ya Taifa
hawatakuwa wakiingia kwenye gharama hizo kubwa kama ilivyo sasa.
“Rais John Magufuli ameshatoa
fedha ili wananchi wasambaziwe huduma ya umeme yakiwamo na maeneo ya
migodi midogo, hivyo naagiza Januari 3, 2021, watu wa Survey wawe
wameshafika kwenye eneo hili la mgodi wa Nyangalata na kuanza mchakato
wa kuleta huduma ya umeme hapa, pamoja na kwenye mgodi wa Tambarare,” amesema Dk. Kalemani.
“Lengo la Rais Magufuli ni
kuwakuza wachimbaji wadogo, ili wachimbe madini kwa ufanisi, na kuongeza
kasi ya uzalishaji wa madini na kupata mapato mengi, na hatimaye kukua
kiuchumi na taifa kwa ujumla, na mkitumia umeme mtaokoa gharama ya
asilimia 80 ya uzalishaji madini ambayo mnaingia kwa sasa na kutumia
Shilingi Milioni 800 kwa mwezi,”ameongeza.
Pia amesema Serikali hadi
kufikia Februari 5, mwaka 2021, wanatarajia kuanza kusambaza pia huduma
ya Nishati ya umeme kwenye vitongoji na vijiji vyote nchi nzima, ambapo
katika wilaya ya Kahama vimesalia vijiji 147, na Halmashauri ya Msalala
kuna vijiji 60.
Katika hatua Nyingine Waziri
Kalemani, akiwa katika kituo cha kupokea umeme, kusambaza, na kupoza
(Substation) kilichopo Bulyanhulu wilayani Kahama, ambacho kinapokea
umeme kutoka Ibadakuli mjini Shinyanga, amekazia suala kukata umeme
hovyo hasa katika Sikukuu ya Mwaka Mpya, na kuonya umeme huo usije
ukathubutu kukatika hata kidogo Mkoani Geita wala kushtua, ambapo kwa
sasa Rais yupo kwenye mapumziko ya Sikukuu hiyo nyumbani kwake Chato.
Naye Mbunge wa Jimbo la Msalala
Iddi Kasimu, amesema kasi hiyo ya usambazaji umeme kwenye makazi ya watu
na maeneo ya migodi, itakuwa ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa
maendeleo kwa wananchi pamoja na wachimbaji wadogo, ikiwamo na kufungua
vitega uchumi vya umeme na kuwaongezea kipato.
Kwa upande wake mmoja wa
wachimbaji wadogo kutoka mgodi huo wa Nyangalata Alex Manyama, amesema
kutokana na kutumia mafuta mazito kuzalisha madini hayo, amekuwa
akitumia kwa siku kiasi cha Shilingi Laki Tisa, na kuomba Serikali
iwapelekee huduma hiyo ya Nishati ya umeme, ili kuwapunguzia matumizi
hayo ya gharama kubwa.
Waziri
wa Nishati Dk. Medard Kalemani, akizungumza na wachimbaji wadogo wa
madini ya dhahabu katika Mgodi wa Nyangalata na kuwahakikishia kuwa
Serikali itawaletea umeme ili kuwapunguzia gharama kubwa za uzalishaji
madini kwa njia ya mafuta mazito na Jenereta.
Mbunge wa Jimbo la Msalala Idd Kasimu akizungumza na wachimbaji wadogo Nyangalata.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha, akizungumza na wachimbaji wadogo Nyangalata.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kahama Thomas Muyonga, akizungumza na wachimbaji wadogo wa Nyangalata.
Wachimbaji wadogo wa madini Nyangalata wakiwa kwenye mkutano wa Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani.
Wachimbaji wadogo wa madini Nyangalata wakiwa kwenye mkutano wa Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani.
Waziri
wa Nishati Dk. Medard Kalemani, akiangalia namna ya uzalishaji madini
ya dhahabu kwa wachimbaji wadogo katika Mgodi wa Nyangalata, kwa kutumia
Jenereta ambapo wanaingia gharama kubwa.
Waziri
wa Nishati Dk. Medard Kalemani, kushoto, akisikiliza maelezo kwa
mchimbaji mdogo Alex Manyama namna wanavyotumia gharama kubwa kuzalisha
madini ya dhahabu kwa njia ya mafuta mazito au Jenereta.
Wachimbaji wadogo wakiwa kwenye shughuli za uchenjuaji madini.
Waziri wa Nishati Dk. Medard
Kalemani, akizungumza kwenye kituo cha kupokea umeme,kusambaza na kupoza
kilichopo eneo la Bulyanhulu wilayani Kahama, kulia ni Mbunge wa Jimbo
la Msalala Iddi Kasimu
Mbunge wa Jimbo la Msalala Iddi Kasimu, akizungumza kwenye kituo cha
kupokea umeme,kusambaza na kupoza kilichopo eneo la Bulyanhulu wilayani
Kahama.
Mkuu wa wilaya ya Kahama
Annamringfi Macha kizungumza kwenye kituo cha kupokea umeme,kusambaza na
kupoza kilichopo eneo la Bulyanhulu.
Mwenyekiti
wa CCM Wilaya ya Kahama Thomas Muyonga, akizungumza kwenye kituo cha
kupokea umeme,kusambaza na kupoza kilichopo eneo la Bulyanhulu.
Waziri wa Nishati Dk. Medard
Kalemani, akisikiliza maelezo kutoka kwa msimamizi wa kituo cha kupokea
umeme, kusambaza na kupoza kutoka eneo la Bulyanhulu Amos Asheli.
Awali Waziri wa Nishat Dk. Medard Kalemani, akiwa kwenye ziara katika mgodi wa madini Nyangalata.
Ziara ikiendelea.
Ziara ikiendelea kwenye kituo cha kupokea umeme, kusambaza, na kupoza katika eneo la Bulyanhulu.
Ziara ikiendelea kwenye kituo cha kupokea umeme, kusambaza, na kupoza katika eneo la Bulyanhulu.
Ziara ikiendelea kwenye kituo cha kupokea umeme, kusambaza, na kupoza katika eneo la Bulyanhulu.
Na Marco Maduhu- Kahama.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...