

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Mashimba Ndaki akimpatia maelezo Waziri wa Mambo ya Nje wa China Mhe. Wang Yi kuhusu samaki wa aina mbalimbali na minofu yao wanaopatikana katika Ziwa Victoria wakati mgeni huyo alipotembelea Mwalo wa Chato mkoani Geita mapema asubuhi ya leo Ijumaa Januari 8, 2021.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Mashimba Ndaki na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Mhe. Wang Yi wakipata maelezo kuhusu minofu ya samaki wanaopatikana katika Ziwa Victoria wakati mgeni huyo alipotembelea Mwalo wa Chato mkoani Geita mapema asubuhi ya leo Ijumaa Januari 8, 2021
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Mhe. Wang Yi akiongea na wavuvi na wadau wengine wa sekta ya uvuvi alipotembelea na mkujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika katika Mwalo wa samaki la Chato Mkoani Geita alikotembelea leo Ijumaa Januari 8, 2021 ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake nchini
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi akimkaribisha rasmi nchini Waziri wa Mambo ya Nje wa China Mhe. Wang Yi na ujumbe wake kabla ya kufanyika mazungumzo rasmi wa pande hizo mbili mjini Chato mkoa wa Geita leo Ijumaa Januari 8, 2021 ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake nchini
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...