Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
KAMPUNI ya Bima ya Afya ya AAR Tanzania imezindua mfumo mpya wa ‘Smart Health Solutions’ ambao utasaidia kusambaza huduma za afya kwa Watanzania wote nchini kiurahisi na haraka zaidi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Afisa Uendeshaji Mkuu wa AAR Tanzania, Dkt. Emmanuel Bona amesema uzinduzi wa mfumo huo ni jitihada za Kampuni hiyo kuunga mkono Serikali kusambaza huduma za Afya kwa Watanzania wote.
Dkt. Bona amesema mfumo huo utawasaidia wadau wengine wa Bima wakiwemo Madalali wa Bima (Insurance Brokers) na Mawakala wa Bima kutoa huduma kwa haraka kwa Wananchi, Kampuni zinazohitaji huduma hizo kwa kutumia Teknolojia.
“Leo tumezindua mfumo huu wa ‘Smart Health Solutions’ ili kuendesha huduma za Bima ya Afya kwa Wadau wote wa Bima, mfumo huu utasaidia watumiaji wa Bima kumpa Mteja gharama ya vifurushi vya Bima wakati akiwa na Mteja bila kurudi kwenye Kampuni ya Bima”, amesema Dkt. Bona.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo, AAR Tanzania, Tabia Massud ameeleza kuwa mfumo huo ni jumuishi kutumika kwa watumiaji wote wa Bima kwa kuanzia na Mawakala wanaouza Bima, Wanachama wa Bima na Wanunuzi.
Tabia amesema mfumo huo wa ‘Smart Health Solutions’ ni rafiki kwa Watumiaji wote ambao unapatikana mahali popote alipo mtumiaji.
Nao baadhi ya Mawakala wamesema wamefurahi kupata elimu kuhusu mfumo huo katika utoaji wa Bima za Afya kwa haraka na kwa urahisi kwa wateja wao.
“Kwa kweli itasaidia sana hasa kwa sisi Mawakala kwa zamani ilikuwa ngumu sana kama kuomba Matibabu unaweza kuchelewa hata kwa siku mbili hadi tatu kwa mfumo huu utatusaidia sana”, amesema Peter Sekidia.
Rose Balyagate amesema imekuwa na manufaa zaidi kwa Mawakala wa Bima kutokana na urahisi wa kutoa majibu kwa haraka zaidi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...