Na Mwandishi wetu, Simanjiro
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, kimewataka
wanachama wake kujitokeza kuchukua fomu za kujaza nafasi zilizo wazi
ikiwemo Katibu mwenezi wa Wilaya na Mwenyekiti wa UWT wa Wilaya.
Katibu
wa CCM wa wilaya ya Simanjiro Ally Kidunda amesema nafasi tano ngazi ya
wilaya zipo wazi na zinatarajiwa kujazwa na wanachama wenye sifa na
nafasi mbalimbali za kata na matawi.
Kidunda
ametaja nafasi za wilaya ni katibu wa siasa na uelezi wa wilaya,
Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa wanawake (UWT) wa wilaya na nafasi
moja ya mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya.
Ametaja
nafasi nyingine ni wajumbe wawili wa halmashauri kuu ya CCM mkoa na
nafasi moja ya mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM kupitia jumuiya ya
wazazi wilaya.
Amesema shughuli za kujaza nafasi zilizo wazi utagusa nafasi zilizo wazi ngazi ya matawi na kata kwa chama na jumuiya zake.
"Nawaagiza
viongozi husika wa ngazi ya kata ya chama na jumuiya kutangaza nafasi
zote zilizo wazi zibandikwe katika mbao za matangazo na maeneo
mbalimbali ya wazi," amesema Kidunda.
Amesema
ratiba ya uchukuaji na urejejeshwaji fomu itakuwa kuanzia Februari 10
hadi 13 mwaka huu kisha mchakato mwingine utaendelea.
Amesema
mapendekezo ya vikao vilivyowajadili wagombea wote yatapelekwa makao
makuu ya Wilaya na taarifa za fomu, mihutasari na mapendekezo zinapaswa
kufika Februari 20.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...