Na Amiri
Kilagalila,Njombe
Kufuatia ununuaji holela wa tunda la parachichi unaoendelea mkoani
Njombe ,mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri amehitaji kupangwa bei elekezi ya
zao hilo ili kuwaepusha na unyonyaji unaoweza kufanywa na wanunuzi kwa wakulima
.
Msafiri amesema kumekuwa na wanunuzi wanaonunua
shilingi 1,200 ,1,500 na wengine 1800 kwa kilo jambo ambalo linaweza kuwafanya
wakulima kukosa tija na maendeleo kwa uwekezaji wanaofanya katika kilimo hicho
chenye soko la uhakika ulimwenguni.
Akizungumza wakati wa hafra ya wadau wa parachichi
waliokutanishwa na asasi ya TAHA kwa kushirikiana na MAKEUP kwa ajili ya
kujadili kuhusu upataji wa cheti cha ithibati ya viwango vya kimataifa GROBAL
GAP na ushuhuda wa baadhi ya wakulima waliopata ithibati. Mkuu huyo wa wilaya
amesema ni vema wafanyabiashara kuwekewa bei elekezi pamoja kuundwa kwa
ushirika ili kudhibiti unyonyaji.
“Kuna changamoto kubwa ambayo mimi naiona inaenda
kuua parachichi badala ya kuiendeleza,wanunuzi kwenda mpaka shabani kwa wakulima
naona ni changamoto kubwa,niwaombe TAHA mtuanzishie masoko ili mkulima akivuna
aende soko lilipo na wanunuzi waje kununulia hapo,hao wanunuzi wanaofuata
mkulima mmoja mmoja hawatendi haki”alisema Ruth Msafiri
Msafiri amesema wakulima wanagawanywa ili mfanyabiashara anunue kwa bei anayoitaka
“Lakini tukiwa na
soko wakulima walete mazao yao wenyewe ndani ya kontena ambazo zimeandaliwa na
anapoleta hapo tunakuwa na soko la kuzindua msimu ili wanunuzi washindane na
wanunue kwa bei nzuri.nashangaa wakulima wamerizika sijapata mkulima hata mmoja
ila mimi moyoni naliona haliko sawa”aliongeza Msafiri
Akifafanua manufaa ya kuwa na vyeti vya ithibati,
kimataifa afisa kilimo,afya ya mimea wizara ya kilimo Musa Chidinda anasema
hatua hiyo itasaidia wakulima wanaoyofanya kilimo biashara kuyafikia
masoko huku Safari Fungo mratibu wa mradi wa MAKEUP akieleza pia faida ya kuwa
na umoja wenye nguvu.
“Zipo faida za kuwa ndani ya Chama cha watu wa
parachichi,na ndio tutaona namna mbinu za kibiashara zitawekwa lakini pia
wasafirishaji wanayo nafasi kubwa ya ushiriki kwenye hili”alisema Safari Fungo
“Pamoja na hilo
tunawasaidi wakulima kupeleka tunda sokoni,mwaka 2020 kwa kushirikiana na TAHA
tuliwapeleka wasafirishaji wa parachichi kwenye maonesho nchini Ujerumani.sasa
hivi tumewasaidi na wakulima wanauza kilo moja kwa dola 10 kutoka dola 2.kwa
hiyo sisi kazi yetu ni kuwasaidia wakulima wapate zaidi matunda kupitia mbinu
za kutafuta ubora lakini pia kuongeza thamani kwenye mazao yao”aliongeza Safari
Fungo
Steven Mlimbila maarufu kwa kilimo cha parachichi
kwa jina la Nemes na Zakia Luwanja ambao ni wakulima wa parachichi wanasema bei
elekezi itasaidia kudhibiti unyonyaji kwa wakulima huku wakibainisha changamoto
ya miundombinu ya barabara na maji kukwamisha uwekezaji wao.
Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri akieleza maono yake juu hujuma wanazoweza kufanyiwa wakulima wa parachichi kutoka kwa wafanyabiashara wanapokwenda kwa mkulima mmoja mmoja mashambani ili kununua tunda hilo.Baadhi ya wakulima na wafanyabiara wa parachichi katika kikao cha semina elekezi juu ya zao la parachcihi kilichofanyika katika ukumbi wa Johnson Holl mjini Njombe.wakifuatilia maelekezo kutoka TAHA na MAKE UP namna bora ya kuendelea kuzalisha tunda lenye ubora.
Moja ya mti wa parachichi katika shamba moja wapo la mkulima mjini Njombe aliyewahi kutembelewa na mwandishi wetu wakati wakulima wengine walipofika kujifunza kilimo bora na cha kisasa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...