Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

Mkuu wa Wilaya Kigamboni Sara Msafiri amewataka wananchi wa Kigamboni kutumia huduma ya maji kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) na kuachana na maji ya visima.

 Aidha, amesema mamlaka pekee iliyopewa dhamana ya kutoa huduma ya maji ni Dawasa, kama mwananchi una kisima chako hautaruhusiwa kutoa huduma ya maji kwa watu wengine

Hayo ameyasema wakati mkutano na wananchi wa Kigamboni akisikiliza kero mbalimbali zinazowakabili ili ziweze kutatuliwa.

Amesema, kumekuwa na kero mbalimbali ambazo aliweza kuzipokea kutoka kwa wananchi kuhusiana na huduma ya maji ya maji inayotolewa na Dawasa na leo wamefika wote kwa pamoja ili kuhakilisha zinaisha 

Mapema wiki iliyokwisha kulikua na Kliniki ya kusikiliza kero za wananchi ndani ya Wilaya ya Kigamboni, kupitia taasisi mbalimbali za kiserikali na kugundua Dawasa inabidi iongeze siku tatu za ziada za kusikiliza kero hizo karibu na maeneo wanayotolea huduma 

"Niliwaambia Dawasa waje maeneo haya wasikilize kero za wananchi lakini nimeambiwa hapa ndani ya siku tatu ni wananchi 25 tu ndo wamefika na kusikilizwa na sisi kama serikali tutayafanyia kazi hayo malalamiko," amesema Sara.

Ameeleza, wananchi wamekuwa na malalamiko mengi wanaongelea pembeni lakini wanapoletewa wahusika ili waelezee kero zao wamekuwa hawafiki jambo ambalo linaamisha kuwa kila kitu kipo sawa na kuishia kuongea pembeni.

"Nimesikia kero ya Bili ya maji na maunganusho mapya, ukiachilia mbali mnataka huduma ya maji Visima kurudishwa niweke wazi Dawasa ndio  mamlaka iliyopewa dhamana ya kutoa huduma ya maji kwa Dar es Salaam na miji ya Pwani, kwa bei elekezi kutoka Ewura," amesema.


"Hivyo msitarajie huduma hiyo kurudi, na hata hao wamiliki wakati wanapewa leseni ili wachimbe visima waliambiwa mtandao wa Dawasa utakapofika basi watasitishiwa huduma hiyo,"


Naye Kaimu Meneja wa EWURA Kanda ya Mashariki Mhandisi Amani Nyekela amesema DAWASA ni moja ya Mamlaka inayofanya nao kazi kwa ukaribu sana.

Akielezea bei ya maji inayotolewa na Dawasa ni elekezi na inatumika kwa maeneo yote ikipitishwa na Ewura.

Akizungumzia miradi ya maji Kigamboni, Meneja Kihuduma Kigamboni Tumaini Muhondwa amesema uendelezaji wa visima hivyo katika mradi wa visima vya Kimbiji utagharimu Bilioni 10.5 kwa fedha za ndani kujenga miundo mbinu na unatarajia kukamilika ndani ya miezi 15.

Amesema, Uendelezaji wa visima umegawanyika katika hatua za ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji, ujenzi na ulazaji wa bomba la kusafirisha majj km 5.7, ujenzi wa kituo cha kupokea maji kutoka kwenye kisimana na ufungaji wa pampu za umeme kwa ajili ya kuendesha mitambo.

Muhondwa ameeleza, kazi ya usanifu imeanza kupitia mshauri WAPCOS na tanki la maji litajengwa eneo la Kichangani kupitia Kisima cha Kifurukwe na ulazaji wa bomba la usambazaji Km 23.9  na utahudumia maeneo ya Kifuruku, Kiziza, Uvumba na Kichangani.

"Sehemu ya pili ujenzi wa bomba kwa umbali wa Km 27 litakalounganishwa na bomba lililovushwa darajani kutoka Ruvu Chini mradi huu utahudumia maeneo ya Kigamboni, Ferry, Tungi, Magogoni na Upendo,"

Mbali na hilo, Dawasa wamewataka wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi katika ofisi zao kwa ajili ya kupatiwa huduma ya maji na kwa sasa wana zaidi ya wateja 3400 wanaopata huduma ya maji safi na salama.
Mkuu wa Wilaya Kigamboni Sara Msafiri akizungumza na wananchi waliojitokeza kwa ajili ya kusikiliza na kutatua changamoto ya Maji ndani ya Mkoa wa Kihuduma Dawasa Kigamboni. wa pili  Kulia ni Meneja wa Wa Dawasa Mkoa wa Kihuduma Kigamboni Tumaini Muhondwa. Mkutano huo umefanyika katika Viwanja vya Swala Wilaya ya Kigamboni.
Meneja wa DAWASA Mkoa wa Kihuduma Kigamboni Tumaini Muhondwa akitoa taarifa ya mradi wa maji wa Kimbiji unaoendelea kutekelezwa na Mamlaka hiyo kwa kutumia fedha za ndani utakaoondoa kero ya maji kwa Mji wa Kigamboni na maeneo ya karibu.


Kaimu Meneja wa EWURA Kanda ya Mashariki Mhandisi Amani Nyekela amesisitiza wananchi kutumia nafasi zao kutoa maoni kupitia njia rasmi ya kupiga simu kwa Mamlaka hiyo ili kuweza kutatua changamoto zinazojitokeza katika sekta ya maji, umeme, gesi na mafuta. EWURA wameshirikiana na DAWASA kuweza kusikiliza na kutoa elimu juu ya huduma ya maji inayotolewa na Mamlaka ya Maji Dawasa Ndani ya Jiji la Dar es Salaam na Miji ya Pwani.

Mkuu wa Wilaya Kigamboni Sara Msafiri akimsikiliza moja ya wananchi waliofika katika Viwanja vya Swala Kigamboni kutoa kero na changamoto mbalimbali.

 





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...