NA  YEREMIAS  NGERANGERA..NAMTUMBO

Diwani wa kata ya Likuyu  wilayani  Namtumbo mkoani Ruvuma ,Kassimu  Gunda  amekasirishwa  na kitendo cha baadhi ya wananchi  kumwekea  jeneza  usiku wa  manane mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Mfuate  nyumbani  kwake.

Bwana Gunda alipata taarifa kwa njia ya simu na alfajiri aliondoka na kufika katika nyumba ya mwalimu huyo  na kulikuta jeneza  lililokuwa linawekwa  msikitini limebebwa  na kuwekwa mbele  ya mlango  wa nyumba ya mwalimu huyo.

Gunda  aliamuru jeneza  hilo kurudishwa msikitini  na kuitisha kikao cha wazee wa kijiji hicho  pamoja na kamati ya shule  kujadili kitendo cha baadhi ya wananchi kumwekea jeneza mwalimu mkuu  wa shule ya msingi Mfuate na kuibua taharuki  kwa walimu.

“Walimu hawa ndio wanaonisaidia mimi diwani kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi  ya kuhakikisha  wanafunzi  kutoka awali mpaka darasa la saba wa shule ya Mfuate wanapata  elimu ,na ili walimu hao wafundishe vizuri  na kutekeleza ilani ya chama  wanahitaji kupata utulivu katika kazi ya kufundisha “alisema diwani huyo.

Mwalimu  mkuu  wa shule  hiyo  bwana  Peter Haule   kwa  upande  wake  pamoja  na kumshukuru  diwani wa kata hiyo namna  alivyompa  ujasiri  wa kuliona tukio hilo kama ni changamoto  katika maisha lakini kabla ya kuja diwani huyo alisema   akili haikuwa  vizuri hasa akilitazama lile jeneza   na alitamani  kufunga  mizigo  yake  na kwenda ofisi ya  mkurugenzi .

Kitendo  cha diwani mwenyewe  kushirikiana na baadhi ya wananchi kuliondoa jeneza kutoka nyumbani  kwake na kufanya  vikao  na wazee wa kijiji hicho pamoja na kamati ya shule  na kumthibitishia kuwa wananchi waliofanya hivyo  wenda  ni  vijana wahuni  na kumthibitishia usalama wake  alipata faraja na kupunguza mawazo aliyokuwa nayo  awali .

Kwa  mujibu wa diwani zoezi  la kuwapata  vijana au wananchi waliofanya kitendo hicho  cha kumwekea mwalimu jeneza  mlangoni  kwenye nyumba anayoishi  wamepewa  wazee  wawili  wa kijiji hicho ambao hakuwataja majina yao na mara watakapopatikana hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ili kudhibiti tabia za ovyo wanazofanyiwa walimu.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...