Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi,ametembelea Shirika la Magazeti ya Serikali (TSN) na kuagiza menejimenti ya taasisi hiyo kuongeza ufanisi kwani kuna watumishi wameanza kuonesha uzembe katika taasisi hiyo.

Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu Dkt. Abbasi, ameagiza kusimamishwa kazi mameneja wawili wa idara za matangazo na usambazaji na eneo la uchapishaji ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi ya idara wanazoziongoza.

"Kila mtumishi wa umma kwa sasa na natoa wito kwa taasisi za Wizara ya Habari ambao najua wengine mlikuwa hamjazoea kuchukuliwa hatua mjue sasa ni saa za kazi; ukileta uzembe kazini utachukuliwa hatua bila kusita," alisema Dkt. Abbasi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...