Na Grace Semfuko MAELEZO

Benki Kuu ya Tanzania BOT imesema hakuna tozo yoyote ya vikundi vidogo vya kifedha vya kijamii (VICOBA) vinavyoendesha shughuli zake, na kwamba hakuna kikundi chochote cha kifedha  kinachomilikiwa na Benki hiyo.

Benki hiyo pia imesema vikundi vya kifedha vya Kijamii ni mali ya Wanachama na kwamba hakuna kikundi kinacholazimika kuwa chini ya makundi mengine kama SACCOS na Taasisi za kifedha.

Hayo yamebainishwa na Meneja Usimamizi wa Mabenki ya Huduma ndogo za fedha na maduka ya kubadilisha fedha za kigeni. Bw. Victor Tarimo, wakati akitoa mada katika Semina kwa Waandishi wa Habari za Fedha, Uchumi na biashara inayofanyika Mkoani Mtwara.

“Hakuna fedha inayotozwa na Benki Kuu ya Tanzania-BOT kwa ajili ya uendeshaji wa kikundi vya kifedha, na hakuna sheria yoyote inayotaka vikundi hivyo vitoe tozo kwenye Taasisi nyingine yoyote, vikundi ni mali ya wanachama na wanaotoza vikundi hivyo kwa ajili ya uendeshaji wanakosea” alisema.

Aliyasema hayo baada ya Waandishi wa Habari kumwambia kuwa kuna baadhi ya Halmashauri za Wilaya na Manispaa wanatoza vikundi hivyo Shilingi elfu 30 kama gharama za uendeshaji wa vikundi.

“BOT tuliwaambia Mamlaka za Halmashauri za Wilaya kuwa, mnaposajili kundi dogo la kifedha, hakuna kutoza pesa yoyote, kama kuna kundi lipo linatozwa fedha sh elf 30 za usajili watuambia, na sisi tutachukua hatua kwa sababu sio utaratibu tuliowapa”alisema

Alisema kutokana na kuona kuna umuhimu mkubwa wa makundi hayo ya Kijamii kujikwamua kiuchumi kupitia mzunguko wa fedha zao wenyewe, BOT iliamua vikundi hivyo visajiliwe bure na kusisitza kuwa  Halmashauri za Wilaya wanalifahamu jambo hilo.

 Meneja Usimamizi wa Mabenki ya Huduma ndogo za fedha na maduka ya kubadilisha fedha za kigeni. Bw. Victor Tarimo, wakati akitoa mada katika Semina kwa Waandishi wa Habari za Fedha, Uchumi na biashara inayofanyika Mkoani Mtwara.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...