MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge amesema ifikapo Alhamisi ya February 25 kituo kipya cha Mabasi yaendayo Mikoani na nje ya nchi cha Mbezi Luis kitaanza rasmi kwa kutoa huduma na kituocha mabasi Ubungo kilichokuwa kikitumika awali hakitotumika Tena.
RC Kunenge amesema hatua hiyo imekuja baada ya kukamilika kwa miundombinu yote Muhimu ikiwemo Majengo, Maegesho, Barabara na ofisi za kutoa huduma.
Aidha RC Kunenge amesema tayari Serikali imekutana na wadau wote husika ikiwemo chama cha Wamiliki wa Mabasi TABOA na wote wamejiridhisha kuwa kituo kimekamilika na kipo Katika Hali nzuri ya kutoa huduma hivyo wapo tayari kutoa huduma.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Sporah Liana amesema ifikapo siku ya Jumanne watafanya kikao na Wafanyabiashara wote watakaokuwa wakitoa huduma ndani ya jengo na siku ya Jumatano watakutana na Wamachinga, Babalishe na Mamalishe kwaajili ya kuwekeana mikakati ya biashara.
Pia Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa amesema Jeshi la Polisi limejipanga kuhakikisha abiria wote wanaosafiri au kuingia kituoni hapo hawapati usumbufu wa aina yoyote.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...