Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.
Dkt. Hussein Ali Mwinyi akisisitiza umuhimu wa Mpango wa Kurasimisha Rasiliamli
na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) katika kuleta ukombozi wa kiuchumi
na kuondoa migogoro ya ardhi visiwani Zanzibar wakati Wajumbe wa Kamati ya
Uongozi ya Mpango huo (Hawapo pichani) walipomtembelea Ikulu
Jijini Zanzibar leo Februari 11, 2021 na kueleza hatua iliyofikiwa katika
urasimishaji ardhi na biashara visiwani
humo.
Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) wakifuatilia hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi walipomtembelea Ikulu Jijini Zanzibar na kufanya naye mazungumzo kuhusu hatua iliyofikiwa katika urasimishaji ardhi na biashara visiwani humo.

Mratibu wa Mpango wa
Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge
Tanzania (MKURABITA) Dkt. Seraphia Mgembe akieleza kuhusu namna wananchi
wa Zanibar wanavyounga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuwaletea ukombozi wa
kiuchumi ikiwemo kuwezesha urasimishaji ardhi na biashara unaofanywa kupitia MKURABITA.

Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.
Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa kwenye picha ya pamoja na Kamati ya Uongozi ya
Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Watumishi na
Menejimenti ya Mpango huo leo Ikulu
Jijini Zanzibar mara baada ya kukutana na Kamati hiyo.
Na
Mwandishi Wetu- Unguja
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa Mpango wa Kurasimisha
Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) una mchango mkubwa
katika kujenga uchumi na kuondoa migogoro ya ardhi baada ya urasimishaji.
Ameyasema hayo leo Februari 11, 2021 Ikulu Jijini
Zanzibar wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na wajumbe wa Kamati ya
Uongozi ya MKURABITA na Menejimenti ya
Mpango huo.
"Nimejulishwa kuwa Mpango huu tangu uanze hapa
Zanzibar, tayari shilingi milioni 441 zimetolewa kuwezesha urasimishaji,
naahidi kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kutoa kipaumbele kwa
kutenga bajeti ili kuendekeza kazi hii ya urasimishaji ",alisisitiza Rais
Dkt. Mwinyi
Akifafanua amesema kuwa mpango wa urasimishaji
utasaidia wananchi wengi zaidi kupata
mitaji ya kukuza biashara na shughuli za uzalishaji.
Aidha, Mhe. Rais Mwinyi amesema Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar itafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na Makamu Mwenyekiti
wa Mpango huo Bi. Immaculata Senje ikiwemo kuendelea kutenga bajeti ya
urasimishaji.
"Mapendekezo yaliyotolewa na Mpango huu ndizo
ahadi zangu za uchaguzi kwa wananchi ikiwemo kuweka mazingira wezeshi kwa
wajasiriamali wadogo ili waweze kufanya kazi zao kwa tija ",alisisitiza
Mhe.Rais Dkt. Mwinyi
Aliongeza kuwa kujengwa kwa vituo jumuishi vya biashara vipatavyo 10 visiwani
Zanzibar kutasadia kuwawezesha wananchi wengi kurasimisha biashara zao na
kuondokana na adha ya urasimu , hii ikiwa ni moja ya ahadi zake wakati wa
uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Akizungumzia ahadi zake kwa wananchi Mhe.Rais Dkt.
Mwinyi amesema kuwa ni pamoja na; kuwezesha wananchi kupata mitaji ambapo
mpango huo unatoa majibu ya changamoto zinazowakabili wananchi katika sekta ya
ardhi na biashara kwa kuwaunganisha na Taasisi za fedha kupitia hati zao za
kumiliki ardhi.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA
Bi. Immaculata Senje amempongeza Mhe. Rais Dkt.Hussein Ali Mwinyi na Mhe. Rais
Dkt. John Magufuli kwa kuchaguliwa na wananchi kwa kura nyingi.
Aliongeza kuwa MKURABITA imepanga kusajili
wajasiriamali 1500, kupima viwanja 5700 katika wilaya za Pemba na Unguja,
kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa urasimishaji ardhi na
Biashara .
Pia, mpango huo utaendelea kuwaunganisha wananchi na
taasisi za fedha ili waweze kukuza mitaji kwa kutumia hati miliki zao za kumiliki
ardhi kujikwamua kiuchumi.
Naye Mratibu wa Mpango huo CPA Dkt. Seraphia Mgembe amesema
kuwa MKURABITA itaendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
kuhakikisha kuwa azma ya kujenga uchumi wa buluu inatekelezwa kwa vitendo ili
wananchi wafurahie matunda ya urasimishaji.
Aliahidi kuendelea kutoa msukumo katika kuwaelimisha
wananchi ili watumie rasilimali ardhi kupata mitaji kupitia hati zao baada ya
urasimishaji.
Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA
wanahitimisha ziara yao Visiwani Zanzibar Februari 12, 2021, Aidha katika ziara
hiyo walishiriki katika ufunguzi wa kituo jumuishi cha Biashara Darajani
Zanzibar, kutoa hati miliki za kumiliki ardhi 50 kwa wakazi wa Shehia ya
Welezo, kuwatembelea wanufaika wa Mpango huo na kujionea shughuli zao na
manufaa waliyopata baada ya urasimishaji.
Ziara ya wajumbe wa Kamati hiyo ilianza Februari
7,2021 na imehitimishwa kwa wajumbe hao kupata fursa ya kukutana na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...