NA YEREMIAS NGERANGERA…NAMTUMBO
Mkurugenzi mtendaji wa Halmasjhauri ya wilaya Namtumbo mkoani Ruvuma Evance Nachimbinya amewaagiza watendaji wa vijiji na kata katika Halmashauri hiyo kukusanya mapato kupitia vitambulisho vya ujasiliamali ,kukusanya mapato yatokanayo na kodi ya majengo pamoja na mabango.
Akiongea na watendaji wa kata na vijiji katika ukumbi wa Halmashauri hiyo Nachimbinya alisema kodi ya majengo na mabango ilikuwa inakusanywa na mamlaka ya Mapato Tanzania TRA lakini kwa sasa serikali imerudisha serikali za mitaa ili kurahisisha ukusanyaji huo .
Hata hivyo bwana Nachimbinya aliwaagiza watendaji hao kuwa kabla ya kuanza ukusanyaji huo watendaji wanatakiwa kuwasilisha taarifa za majengo yanayostahili kulipiwa kodi pamoja na idadi ya mabango yanayotakiwa kulipiwa yaliyopo katika vijiji vyao katika ofisi ya mkurugenzi .
Awali afisa biashara wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo bwana Revocatus Kavishe aliwaambia watendaji hao kuwa wanatakiwa kufuata sheria taratibu na kanuni katika kusajiri walipa kodi za majengo na sio kupokea maelezo ambayo yanayolenga kukwepa kulipa kodi na kimsingi hayapo katika sheria.
Kavishe alidai uzoefu unaonyesha kuwa wapo watendaji katika kutekeleza majukumu yao huwa hawasimamiii kanuni na sheria zilizopo na badala yake husikiliza maelezo ya watu wenye nia ya kukwepa ambayo hayapo katika kanuni na sheria zilizopo .
Alitaja uzoefu alioupata katika ukusanyaji wa fedha za vitambulisho vya ujasiliamali alidai wapo watendaji ambao hawakuuza vitambulisho kwa baadhi ya wafanyabishara wadogo kutokana na kusikiliza maelezo na kuacha kuwauzia vitambulisho badala ya kufuata sheria na kanuni zilizopo za wanyasiliamali wote wanahitajika kuwa na vitambulisho badala ya kupokea maelezo.
Mario Mwageni mtendaji wa mamlaka ya mji mdogo wa Namtumbo kwake yeye zoezi hilo alidai sio geni lakini alihoji sheria ya ukusanyaji inasemaje katika maeneo mengine ambayo sio mamlaka ya miji midogo kwa kuwa ukusanyaji katika sheria inayotumika inaishia kukusanya kodi ya majengo mwisho katika mamlaka ya miji midogo pekee.
Afisa kodi ya majengo kutoka mamlaka ya mapato wilaya ya Namtumbo bwana Samwel Masawe aliyehudhuria kikao hicho alidai nyumba zinzotakiwa kulipiwa kodi ya jengo ni zile zilizojengwa kwa tofali na kuezekwa bati huku ndani ya nyumba hizo kuna watu wanaishi. Alifafanua bwana Masawe.
Afisa utumishi wa Halmashauri hiyo Eleonora Lyimo pia alitumia nafasi hiyo kuwataka watumishi kuitisha vikao kwa mujibu wa sheria huku akiwasihi kufanya kazi zinazowapasa kufanya na kuacha kujiingiza katika makundi ya siasa pamoja na kujikita katika swala la ulevi kupindukia na kusahau kazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...