* Ujio walenga kukutana na wadau wa Elimu
Na Mwandishi Wetu
MKURUGENZI wa Global Link Education(GEL) Abdulmalik Mollel ameelezea umuhimu wa ujio wa Profesa Dmitry Savkin kutoka Irkutsk National Research Universty atakayekuwa nchi Tanzania kwa siku kati ya 13 hadi 14 kuanzia Ijumaa ya wiki iliyopita.
Akiwa nchini Profesa Irkutsk atatembelea vyuo mbalimbali nchini na kukutana na wadau wa elimu nchini kwa ajili ya kujadili masuala yanayohusu sekta ya elimu na kubwa zaidi ni namna ya kushirikiana katika eneo hilo baina ya vyuo vya Tanzania na Dmitry Savkin Universty nchini Urusi.
Akizungumza na Michuzi TV jijini Dar es Salaam, Mollel amesema Profesa Savkin anatoka kwenye chuo hicho ambacho kina uzoefu katika utoaji wa elimu ya juu kwa zaidi ya miaka 90 katika nchi hiyo ni moja ya vyuo ambavyo vimewekeza kwenye teknolojia.
"Chuo hicho kinatoa mafunzo kwenye kozi mbalimbali zikiwemo masuala ya anga, utengenezaji wa ndege, biashara, uhasibu na aina nyingine ya kozi zote zinahusu teknolojia na kwa sasa ni Vice -Rector for International Affairs Dean of Baikal School of Brics na atakuwa nchini kwa siku 13 hadi 14.
"Lengo kubwa la ujio wake ni kuangalia jinsi gani ambavyo wanafunzi au vyuo vya Tanzania vinavyowezesha kushirikiana kwa karibu na Chuo chake pamoja na vyuo vingine vya nchini Urusi na vile vyuo ambavyo wana ushirikiano navyo katika mataifa mbalimbali duniani,"amesema Malik.
Ameongeza chuo hicho kina teknolojia ya hali ya juu, hivyo kitakapokuwa na ushirikiano na vyuo vya Tanzania kuna faida kubwa ambayo wanafunzi waliopo nchini watakaipata ikiwemo ya kunufaika na teknolojia ambayo wataipata.
"Kama mnavyofahamu gharama kwenye chuo hicho ni za kawaida hasa kwa kuzingatia nchini Urusi kuna vyuo zaidi ya 1000. Atakapokuwa nchini atatembelea Mikoa mbalimbali na ataanza na Zanzibar kwa kutembelea vyuo kadhaa na kukutana na wadau wa elimu.
"Baada ya hapo atakwenda mikoa ya Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma na kisha kumalizia jijini Dar es Salaam na kote huko atakutana na wanafunzi na wadau wa elimu ya vyuo vikuu kujadiliana namna bora ya kushirikiana katika sekta ya elimu kati ya Tanzania na Urusi na mataifa mengine."amesema Mollel.
Aidha amesema Profesa huyo atakapokuwa nchini watajadiliana namna ya kuweka nguvu katika sekta ya utalii ambapo kupitia vyuo vikuu, Tanzania inaweza kuwa inapata wanafunzi kutoka Urusi ya Ukraine ambapo watakuwa wanakuja nchini kimafunzo na hiyo itakuwa fursa katika kuongeza idadi ya watalii nchini.
"Tunataka wanafunzi kutoka kwenye chuo hicho cha Urusi pamoja na vyuo vingine waje nchini kwenye programu za kimafunzo zikiwemo zinazohusu masuala ya tafiti na vijana hao watakapokuja nchini watafanya na utalii , hivyo itakuwa fursa kwetu katika kukuza sekta ya utalii nchini kwani watakaporudi makwao watakuwa mabalozi wazuri wa kulitangaza jina la Tanzania.
"Nchi ya Urusi imekuwa ikipeleka maelfu ya wanafunzi wake kwenye mataifa mbalimbali duniani yakiwemo ya China,Japan Canada Ukraine pamoja na mataifa mengine, hivyo kwanini tusitumie nafasi hii kuweka ushirikiano wa wanafunzi hao kuja kwetu,"amesema.
Amesema hivyo ni vitu ambavyo wamevijadili na kukubaliana , kwani hakuna sababu ya wanafunzi wa Tanzania tu kuwa ndio wanakwenda kwenye nchi hizo bali umefika wakati na wao kuja nchini kwa ajili ya programu mbalimbali za kimafunzo.
Aidha amesema kuna programu nyingi zinazofundishwa na chuo hicho hicho na nyingi zinakuwa za miaka minne lakini miaka miwili wanafundisha nchini kwao na miaka miwili wanamalizia kwenye nchi nyingine.
"Hizi programu tunaziita doble degree, kwani unakuwa na cheti kutoka kwenye nchi yao ya Urusi na unakuwa na cheti kutoka katika nchi nyingine. Na kozi hizo zinasaidia katika kujenga uzoefu wa kimataifa kwa mwanafunzi.
"Hivyo kupitia programu hizo tunachukua wanafunzi wanasoma nchini Tanzania mwaka mmoja
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...