Na Farida  Saidy, Morogoro.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amewataka wajumbe wa Bodi za Shule za Sekondari Mkoani hapa kutowafumbia macho Wanafunzi wote wanaokiuka taratibu na maadili ya Shuleni,kwani kufanya hivyo kutasaidia kuongeza nidhamu baina ya Wanafunzi na waalimu na kuongeza ufaulu.

Loata Sanare ameyasema hayo February 19 alipokuwa anapokea Madawati na viti 110 kutoka  Benki ya NMB,ambao amesema Serikali  ya awamu ya tano pamoja na wazazi wanahangaika kwa ajili ya watoto wao wapate elimu,hivyo si vyema kwa Wanafunzi kuacha masomo na kujihusisha na masuala yasio na madili.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa huyo ametoa pongezi kwa NMB  kanda ya Mashariki kwa kuwa na Utamaduni wa kuunga Mkono juhudi za Serikali katika kuleta maendeleo  hususan katika sekta ya elimu

Naye Diwani wa Kata ya Kilakala Marco Kanga amewataka walimu na menejimenti za Shule zilizopata msaada  wa viti na Madawati kutunza miundombinu hiyo ili iwasaidie kwa muda mrefu.

Shule zilizopokea msaada huo ni Shule ya Sekondari ya Lupangailiyoko Kata ya Kilakala na Shule ya Sekondari ya Kihonda Kata ya Mazimbu.

Meneja wa benki ya NMB  kanda ya Kati Dismas Prosper akimkabidhi Madawati na viti Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare kkwa ajili ya Shule za Sekondari za Lupanga na Kihonda.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...