Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mwanaidi Ali Khamisi amezindua jengo la kusomea Wanafunzi (Study Lobby) la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) katika Ofisi za Bodi hiyo zilizopo Mhasibu House jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huo, Mhe Mwanaidi amesema ni utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025, amesema ahadi ya Rais Magufuli alieleza mkakati wa Serikali ya awamu ya tano katika Sekta ya Elimu mpango wa kukarabati, kujenga miundombinu  yake.

Mhe Mwanaidi amewapongeza Bodi ya NBAA katika kutekeleza majukumu yao hasa katika maandalizi mazuri ya mazingira kwa Wanafunzi hao. 

"Wanafunzi sasa kazi kwenu, mnapaswa kusoma sana mjitahidi ili mfaulu vizuri masomo yenu", amesema Mhe Mwanaidi.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NBAA, CPA (T) Dkt Neema Msusa amesema NBAA tangu kuanzishwa imetoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya Elimu hususan katika Taaluma ya Uhasibu, amesema ina chochea kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa Uchumi nchini na duniani kwa ujumla.

Dkt Msusa amesema NBAA ina Maktaba yenye uwezo wa kuchukua Wanafunzi 150 pekee, wakati wa mitihani nafasi hiyo ina kuwa finyu, hivyo uzinduzi wa Jengo hilo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa ufinyu wa nafasi kwa Wanafunzi.

Hata hivyo, Serikali na Bodi ya NBAA imetoa pongezi za dhati kwa Mfadhili wa Mradi wa Jengo hilo kwa asilimia 100, Dkt B.S Sreekumar ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Unique Academy.

Naibu waziri wa Fedha na Mipango, Mwanaidi Ali Khamis(Mb) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa jengo la kusomea wanafunzi(Study Lobby) lililopo katika ofisi za NBAA jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu(NBAA), CPA Pius Maneno, kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NBAA, CPA Dkt.Neema Msussa na wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Unique Academy na Mfadhili wa Mradi wa Jengo la kusomea wanafunzi(Study Lobby), Dkt. B. S. Sreekumar.
Naibu waziri wa Fedha na Mipango, Mwanaidi Ali Khamis(Mb) akisoma hotuba yake kuhusu namna Serikali inavyoshirikiana na wadau mbalimbali katika sekta ya elimu wakati wa uzinduzi wa jengo la kusomea wanafunzi(Study Lobby)lililopo  katika ofisi za Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu(NBAA)  jijini Dar Es Salaam leo.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NBAA, CPA Dkt.Neema Msussa akisoma hotuba kwa mgeni rasmi kuhusu kazi zinazofanywa bodi hiyo pamoja na namna walivyosimamia ujenzi wa jengo la kusomea wanafunzi(Study Lobby) litakalowawezesha wanafunzi wanaosoma kwa ajili ya mitihani ya bodi hiyo kutopata shida wakati wa uzinduzi wa jengo hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu(NBAA), CPA Pius Maneno akitoa neon la ukaribisho na kueleza kwa ufupi namna mradi huo ulivyotekelezwa na Mfadhili wa Mradi Dkt. B. S. Sreekumar wakati wa uzinduzi wa jengo la kusomea wanafunzi(Study Lobby) lililopo katika ofisi za NBAA jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Unique Academy na Mfadhili wa Mradi wa Jengo la kusomea wanafunzi(Study Lobby), Dkt. B. S. Sreekumar akizungumzia namna alivyoguswa na kufanikiwa kujenga jengo la kusomea wanafunzi(Study Lobby) litakalowahudumia wanafunzi wengi wanaosoma kwa ajili ya mitihani ya Bodi.
Naibu waziri wa Fedha na Mipango, Mwanaidi Ali Khamis(Mb) akimkabidhi zawadi kwa niaba ya uongozi wa Bodi ya NBAA Mkurugenzi Mtendaji wa Unique Academy na Mfadhili wa Mradi wa Jengo la kusomea wanafunzi(Study Lobby), Dkt. B. S. Sreekumar kwa kutambua mchango wake katika Bodi hiyo wakati wa uzinduzi wa jengo la kusomea wanafunzi(Study Lobby) lililopo katika ofisi za NBAA jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NBAA, CPA Dkt.Neema Msussa (kushoto) akimkabidhi zawadi mgeni rasmi Naibu waziri wa Fedha na Mipango, Mwanaidi Ali Khamis(Mb) kwa kutambua mchango unaotolewa na Bodi hiyo wakati wa uzinduzi wa jengo la kusomea wanafunzi(Study Lobby) lililopo katika ofisi za NBAA jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu(NBAA)  pamoja na wadau mbalimbali wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Naibu waziri wa Fedha na Mipango, Mwanaidi Ali Khamis(Mb) wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo la kusomea wanafunzi(Study Lobby).
Naibu waziri wa Fedha na Mipango, Mwanaidi Ali Khamis(Mb) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu(NBAA) wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo la kusomea wanafunzi(Study Lobby).
Naibu waziri wa Fedha na Mipango, Mwanaidi Ali Khamis(Mb) pamoja na viongozi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu(NBAA)  wakiwa kwenye picha ya pamoja na familia ya Mkurugenzi Mtendaji wa Unique Academy na Mfadhili wa Mradi wa Jengo la kusomea wanafunzi(Study Lobby), Dkt. B. S. Sreekumar wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo la kusomea wanafunzi(Study Lobby).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...