Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (ICT) - Mhe. Mhandisi. Andrea Mathew Kundo pamoja na Maafisa wa wizara hiyo pamoja na maafisa kutoka UCSAF, TCRA-CCC, TCRA, wakizungumza na Wajumbe wa Kamati Tendaji ya Vodacom Tanzania PLC, wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Hisham Hendi (kwenye runinga) wakati wa ziara ya naibu waziri, alipozuru makao makuu ya Vodacom Tanzania jijini Dar es salaam. Lengo la ziara hiyo likiwa ni kufahamiana pamoja na kujadili njia za kuongeza thamani ya mteja na kuhakikisha ufanisi wa utendaji.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mtandao cha kampuni ya Vodacom Tanzania PLC, Andrew Lupembe akizungumza kwenye mkutano huo kuhusu namna kampuni hiyo inavyoendelea kutanua na kuboresha mtandao wake ili kutoa huduma bora kwa wateja wa kampuni hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...