Na Khadija Seif,Michuzi Tv
TAMASHA la "Dance Away" limejipanga kukata Kiu ya Wapenzi wa Burudani ya Muziki wa Live Band.
Tamasha hilo ambalo liameandaliwa na Kampuni ya Horrivert Ikishirikiana na '361 Degree' imepanga Kuwakutanisha Wakali Mbalimbali akiwemo Mkali wa Kibao Cha Sea 'Nguza Viking,Kassim Mganga,Nedy Music pamoja na Banana Zorro Sambamba na Band yake ya 'The B Band Februari 14 mwaka huu Ikiadhimisha Siku Ya Wapendanao Katika Hoteli Ya Sea Cliff Jijini Dar es salaam.
Hata hivyo Gwiji huyo wa Muziki Nguza Viking amesema amejipanga kukata kiu Mashabiki zake ipasavyo.
"Tangu nipate Msamaha wa Rais wetu Kipenzi cha Wanyonge,Hafla hii itakua ndio ya Kwanza Kufanya Onesho na itaashiria rasmi Kurudi kwangu kwenye Uwanja wa Muziki "
Pia Viking amewaomba Mashabiki Wa Muziki wa Live Wasikose Kufika Kwa wingi Katika Hoteli Ya Sea Cliff Masaki Kujumuika Kwa pamoja Katika Siku hiyo Ya Wapendanao.
Amemtaja Kassim Mganga Kama Msanii ambae anafanya Muziki Mzuri Kwa Sasa na baadhi ya Vibao Vyake Vimekua Vikimkuna Kutokana na Umahiri Wake Wa Kutunga Mashairi yake .
"Wote tunajua Uwezo wa Kassim Mganga Wa Kutunga,Kuimba pamoja na Kutumbuiza hivyo Basi Kwa Mara ya Kwanza Tutaimba Wimbo Wetu Wa "Harusi yangu".
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...