Mkurugenzi Mtendaji  Dorie ainisha mikakati mbalimbali ya Shirika hilo.


Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv

 Shirika la Taifa la Bima (NIC) limezindua bidhaa mpya ya Bima kubwa ya Flex ambayo itatoa fursa kwa Taasisi au kikundi kukata Bima  hiyo kwa kulipa kidogo kidogo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bima hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Dkt.Elirehema Dorie amesema Bima hiyo inafaida kubwa kwa wenye magari katika Taasisi,Kampuni au kikundi kwa kuzingatia mahitaji yote wakati gari ikiwa imepata ajali.

Amesema Bima ya Flex inatoa nafasi ya kulipa hadi mtu wa tatu katika ajali pamoja na kulipa majeruhi.

Amesema bima hiyo kwa wateja wake wakati gari ikiwa imepata ajali ikiwa matengenezo mteja atalipwa sh.50,000 kwa wiki tatu ambapo gari litakuwa tayari limeshatengenezwa.

Dorie amesema kuwa ulipaji wa Bima hiyo  kidogo kidogo hakuna riba watakayotoza lengo ni kuona wateja hawapati usumbufu.

Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema Shirika limeamua kubadilika kwa kwenda kasi na Mipango ya Serikali kwa baada ya miaka 10 ijayo asilimia 50 watanzania wawe na bima.

Amesema kuwa Shirika litaendelea kutoa elimu ya Bima kwa njia yeyote lengo ni kutaka watanzania wawe na uelewa bima katika kutatua changamoto zao.

Amesema wataendelea kutoa bidhaa mbalimbali za Bima kwa kila eneo kutokana wao wabobezi katika eneo hilo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Dkt.Elirehema Dorie akizungumza wakati uzinduzi wa Bima kubwa ya Flex ,uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Dkt.Elirehema Dorie (mwenye tisheti nyeusi)akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi Bima kubwa ya Flex uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Masoko wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Yesaya Mwakifulefule akitoa maelezo kuhusiana na Bima kubwa ya Flex katika soko la Bima nchini katika uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja Bima Uandikishaji wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Emmaculate Mweteni akizungumza kuhusiana na bidhaa ya Bima kubwa ya Flex walivyojipanga kuiuza kwa wateja.

 Sehemu ye meza kuu,baadhi ya wafanyakazi wa NIC na mawakala wa Bima wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika uzinduzi wa bidhaa ya Bima kubwa ya Flex

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...