Na MWAMVUA MWINYI,PWANI
JESHI
la Polisi mkoani Pwani limetoa madawati (viti na meza) 50 vyenye
thamani ya shilingi milioni nne ili kukabiliana na changamoto ya
upungufu wa madawati,Mkoani hapo.
Kamanda
wa polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa akikabidhi vifaa hivyo kwa mkuu
wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ameeleza wanaunga mkono
jitihada za Rais Dk John Magufuli katika kuboresha na kupambana na
changamoto kwenye sekta ya elimu.
Nyigesa alisema nao ni wazazi wanaona jinsi gani watoto wao wanavyotaabika kutokana na upungufu wa madawati.
"Sisi
mbali ya kulinda wananchi na mali zao pia tunaisaidia jamii kwenye
changamoto mbalimbali zinazowakabili kwani nasi tunamchango wa
kuiwezesha jamii," alisema Nyigesa.
Alieleza,wanakabidhi madawati hayo kwa mkuu wa mkoa ambaye naye atayapeka kwenye shule ambazo zina upungufu mkubwa wa madawati.
"Tunaomba
tukukabidhi madawati haya ambayo ni michango yetu kwa lengo la
kuisaidia jamii hususani kwenye sekta ya elimu ili kukabili changamoto
hiyo ya upungufu wa madawati," alisema Nyigesa.
Kwa
upande wake mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo alilipongeza
jeshi hilo kwa kutoa msaada wa madawati hayo kwani yatasaidia kuboresha
sekta ya elimu.
Ndikilo alisema
itakuwa chachu kwa wanafunzi kuwa raia wema wanapoona polisi inatoa
misaada mbalimbali kwa jamii,na amehimiza jamii kushirikiana na polisi
kufichua wahalifu na kutoa taarifa za uhalifu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...