Na Linda Shebby, Pwani
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia mtuhumiwa mmoja mwanaume Shaaban Rashid Athumani mwenye umri wa miaka 61 mkazi lwa Kwamakocho , Kata ya Mamdela Wilayani Chalinze Mkoa wa Pwani kwa kosa la kumili Kiwanda cha kutengeneza silaha za kienyeji(gobole).
Yamesemwa hayo na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani (RPC), Nyigesa Wankyo kwamba mnamo Januari 31 mwaka 2021 majira ya saa moja usiku katika eneo tajwa hapo juu , Jeshi la Polisi lulimkamata akiwa na vifaa vya kutenfengezea silala aina ya gobole na vingine ikiwa ni pamoja na Mtambo wa kufulia vyuma,chupa tano na ndogo zenye baruti ndani yake,faraki 48,risasi 42 za bunduki aina ya gobole, paketi moja ya unga wa kiberiti,mitambo mitatu ya silaha aina ya gobole, ambayo ipo tayari bado kuwekwa kwenye silaha aina ya gobole na kopo moja lenye tindikali ambao una tumika kuunganisha vyuma vinavyifungwa kwenye silaha aina ya gobole.
RPC Wankyo amesemamkuwa pia jeshi hilo
limekamata limekamata silaha na risasi zake" mnamo Januari 21 mwaka huu majira ya saa 6:30usiku katika maeneo ya Pingi Wilaya ya Kipolisi Chalinze Mkoa wa Pwani walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja jina limeifadhiwa kwa kosa la kumiliki bunduki tatu Shortgun mbili na gobole moja , risasi 13 za shortgun, maganda matatu ya risasi, coocking handle mbili, goroli 60,misumeno miwili ya kukatia mbao na chuma, pia alikamatwa na Plaizi moja , bisibisi moja, kipande cha mtutu wa bunduki, vipande vidogo vya vyuma sita, vipande vya miti vyenye chuma ndani vinne, mitambo ya kutengenezea bunduki viwili, juhudi za kuwatafuta watuhumiwa wengine katika tukio hili zinaendelea alisema RPC Wankyo.
Aidha RPC Wankyo aluongeza kwa kusema kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linawashikilia watuhumiwa wawili wote wanaume amvao ni Mtuli Mhode Chapalisi mwenye umri wa miaka (52) kabila Mmasai na Reuben Krekereni Oyela mwenye umri wa miaka( 31) kabila Masai ,mtuhumiwa mwingine ni Hamisi RongwinyoChambuli mwenye umri wa miaka( 67) wote hawa ni wafugaji kwa kosa la kung'oa na kuharibu mazao (miche ya mikorosho) kwenye shamba lenye ukubwa hekari saba mali ya Reuben Mkandala na John Simon Biginagwa (marehemu kwa sasa) aliyekua mtumishi katika ofisi ta Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
Kwa pamoja watuhumiwa hao na wenzao ambao bado wanatafutwa waling'oa miche hiyo katika shamba tajwa Januari 27 mwaka huu saa nane mchana katika kitongoji cha Ribaya , Kijini cha Diozile Wilaya ya Kipolisi Chalinze Mkoa wa Pwani na kusababisha hasara ya 50,000,000.
Wakati huohuo RPC Wankyo amesema kuwa kumerokea ajali ambapo gari imeacha njia nan kupinduka na kusababisha uharibifu wa gari.
"Ajali hiyo imetokea jana Januari mosi mwaka huu majira ya saa mbili usiku huko Mdaula Wilayani Chalinzr Mkoa wa Pwani ambapo gari lenye namva T.991DFH Howo lenye trela T. 801CLM lililokuwa limebeba mafuta aina ya dizeli likiendeshwa na dereva Masoud Abdallah mwenye umri wa miaka (46) kavila Mnyiramva Mkaazi wa Kimara Jijini Dar es Salaam.
"Alipata ajali hiyo akitokea Dar es Salaam kwenda Zambia baadanya kuacha njia na kupinduka na kusababisha uharibifu wa gari hilo, chanzo cha ajali ni dereva kuendesha gari huku akiwa amelewa pombe,baada ya kupekuliwa kwenye gari alikutwa na pombe aina ya K- Vant iliyokua imetumika na chupa , Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wananchi kuacha uhalifu na kuacha kuendesha vyombo vya moto huku wakiwa wamelewa"
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...