
Diwani wa Kata ya Kivule Nyasika Getama akizungumza January 30/2021katika kikao cha Serikali ya Mtaa Kivule ambapo alialikwa kuwa mgeni rasmi, katika hotuba yake Diwani Nyasika alielezea kukuza sekta ya Elimu na kuwaimiza WANANCHI kukata Bima ya Afya iliyoboreshwa kwa ajili matibabu.


Na Heri Shaaban
SERIKALI ya Mtaa Kivule inatarajia kufungua soko la Kivule February Mwaka huu kwa Wafanyabiashara wote wa kata hiyo.
Akizungumza katika mkutano wa adhara ulioandaliwa na Serikali ya Mtaa Kivule Halmashauri ya Ilala Dar es salaam jana ,Mwenyekiti wa Mtaa Kivule Amos Hangaya alisema alhamisi Febuary 4 Mwaka huu wanawaita Wafanyabiashara wote kwa ajili ya kuwatambua upya pamoja na kugawa vizimba vya Biashara amewataka wafanyabiashara wote kujitokeza siku hiyo.
Mwenyekiti Amos alisema kwa sasa soko hilo litatumika kwa dhumuni lililolusudiwa soko sio Mnada,Gulio watawatafutia utaratibu kwa ajili ya kuendesha minada yao kila wiki.
"Nawaomba Wafanyabiashara wote ambao walipewa vizimba katika soko hili kujitokeza siku hiyo kwa ajili ya kuwatambua rasmi soko linataka kufunguliwa hivyo wote mnatakiwa kufanya biashara sehemu rasmi ambazo zimetengwa na sio mitaani au barabarani " alisema Amos.
Amos alisema Serikali ya awamu ya tano TANZANIA ya Uchumi wa viwanda inayoongozwa na Rais John Magufuli inataka wananchi wake wafanye biashara ili wajikwamue kiuchumi sambamba na kuunda viwanda vidogovidogo ili wapate kipato.
Aliwataka wakazi wa Kivule kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli katika kufanyaji kazi na kuleta maendeleo pamoja na kusimamia miradi ya Serikali ambayo ipo katika eneo hilo.
Wakati huo huo Mwenyekiti Amos alisema moja ya Mikakati yake mingine kuanzisha ruti mpya ya Daladala Kivule Sokoni kwenda Mnazi Mmoja inatarajia kuanza Wiki hii nauli bei yake shilingi 400/= na ukipanda ufikishwe mwisho wa gari usikubali kushushwa njiani kwa ili wakatishe ruti.
Amos alisema utaratibu wa ruti hiyo daladala hizo umeshakamilika kila abiria akipanda adai tiketi jambo lolote likitokea atoe taarifa
Mamlaka husika.
Kwa upande wake Mgeni rasmi Diwani wa Kata ya Kivule Nyasika Getama aliunga mkono juhudi hizo hatawasaidia ili malengo yaweze kutimia
Diwani Nyasika aliwataka WANANCHI wa Kata hiyo kukata bima ya afya kwa ajili matibabu kwani maisha ya mwanadamu matibabu gharama kubwa hivyo kuna umuhimu wananchi wa kata ya kivule wote wawe na Bima ya afya
Alisema kwa sasa Serikali imerahishisha imetoa Bima iliyoboreshwa kwa ajili ya wananchi wote kuanzia ngazi ya familia hadi mtu mmoja.
Akielezea sekta ya elimu alisema kata ya Kivule ipo Ilala Vijijini matokeo ya mwaka huu shule ya sekondari wamepata alama A ufaulu mzuri na maadili kitaaluma yapo vizuri amewataka wazazi kufatilia maendeleo ya watoto wao na kushirikiana na Walimu wa Msingi na Sekondari.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...