Wawakilishi wa Michuano ya Klabu Bingwa Afrika Simba inashuka dimbani usiku wa leo kumenyana klabu ya As Vita ya DR Congo katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Martyrs jijini Kinshasa.

Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes kitashuka dimbani majira ya saa 4 usiku kwa saa za Afrika Mashariki ikiwa ni mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi.

Gomes ameweka wazi kuwa anatambua mchezo huo ni mgumu sana ukizingatia uzoefu wa wachezaji wengi wa As Vita sambamba na mbinu za Kocha Mkuu wa AS Vita, Florent Ibenge.

Amesema, anaamini wachezaji wake watapambana ili kupata matokeo chanya na kujinyakulia  pointi tatu muhimu.


Aidha, Simba katika msimu wa mwaka juzi wakiwa wanashiriki michuano hiyo ya kimataifa, waliweza kupoteza mchezo wao dhidi ya As Vita kwa mabao 5-0.

Hiki ni kikosi ambacho kinatarajiwa kuanza leo mbele ya AS Vita ugenini:-

Aishi Manula

Shomary Kapombe

Joash Onyango

Ame Ally

Erasto Nyoni

Thadeo Lwanga

Mzamiru Yassin

Junior Lukosa

Luis Miquissone

Clatous Chama

Benard Morrison

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...