Mtendaji Mkuu wa GST Dkt Mussa Budeba ameongea na vyombo vya habari juu ya mafanikio mbalimbali ya tafiti za awali za jiosayansi ilizofanya katika sehemu mbalimbali za nchi ambazo ndio chanzo cha migodi ya madini nchini.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo katika banda la maonesho la GST lililopo katika Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere kilichopo Jijini Dar es salaam.
Sambamba na Dkt Budeba wataalam wengine waliozungumza ni pamoja na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Kanzi Data GST , Bi Yokbeth Myumbilwa , Mjiolojia waandamizi John Kalimenze na Kaimu Mkurugenzi Huduma za Maabara GST Notka Banteze.
Nguli wa Sheria nchini Kenya, Patrick Luch Otieno Lumumba (P.L.O Lumumba) ametembelea Banda la GST lililopo katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini nchini 2021 unaoendelea katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...