Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
TANZANIA imeendelea kung’ara katika Soka la Kimataifa baada ya Namungo FC kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya ushindi wa jumla ya bao 7-5 dhidi ya Clube Desportivo 1º de Agosto ya Angola katika mchezo wa maraudiano wa michuano hiyo uliopigwa kwenye dimba la Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.
Licha ya kichapo cha bao 1-3 katika mchezo wa marudiano uliopigwa Februari 25, 2021 Namungo itaendelea kuwakilisha Taifa la Tanzania katika michuano ya Kimataifa hatua ya makundi. Mchezo wa mkondo wa kwanza Namungo walishinda bao 2-6 katika uwanja huo huo wa Chamazi.
Baada ya ushindi huo katika michezo yote miwili iliyochezwa nchini Tanzania, Namungo sasa wanaangukia Kundi D linalojumuisha timu za Raja Casablanca ya Morocco, Pyramids FC ya Misri na Nkana Red Devils ya Zambia.
Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Hassan Zidadu amekiri changamoto zilizowakumba nchini Angola zimewafunda mambo mengi zaidi wakati wakiendelea kushiriki Michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho Afrika.
“Angola tumekutana na mambo yale, Je huko tunapoenda sasa hivi kwenye makundi kutakuwaje? huko tunapoenda sasa hivi tutajihami kwa sababu tulishapitia magumu,” amesema Zidadu
Kocha Mkuu wa Namungo FC, Hemed Suleiman Morocco amesema michezo kadhaa dhidi ya timu za Sudan, Angola waliyoipata katika michuano hiyo itawasaidia katika hatua ya makundi ya CAF.
Namungo FC imefuzu hatua hiyo ya makundi sambamba na Simba SC waliofuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kupeperusha vyema bendera ya Taifa katika michuano hiyo ikiwa Kundi A na timu za Al Ahly SC, AS Vita Club na Al-Merrikh SC.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...