TECNO Mobile ni moja ya kampuni iliyoshiriki vyema katika kuonyesha upendo kwa wateja wake.
TECNO ilizindua rasmi promosheni ya valentine (TUNAKUTHAMINI MTHAMINI) maalumu kwajili ya kujumuika na wateja wake katika usiku wa valentine.
Katika usiku wa valentine wateja wa TECNO wakiwa na wapenzi wao walipata chakula cha usiku katika Hotel ya kifahari Serena beach huku kila mualikwa akionekana kufurahia wakati huo.
TUNAKUTHAMINI MTHAMINI ni promosheni iliyolenga zaidi wateja wa TECNO Spark 5pro walionunua simu hizo na katika msimu huu wa wapendanao. TECNO Spark 5pro ni simu mpya katika tokeo la TECNO Spark na sifa yake kubwa ni vile ambavyo inaweza kuchukua picha au kuangalia video kupitia kioo kipana cha nchi 6.6 na battery ya ujazo wa mAh 5000 yenye kukaa na chaji kwa muda mrefu na memory ya ukubwa wa GB3/64 ya kuhifadhia picha, video na files nyengine nyingi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...