Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
NI rasmi sasa Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) limevunja mkataba na Kocha Etienne Ndayiragije kuinoa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ikiwa ni siku chache timu hiyo kuondolewa kwenye Michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza Ligi za Ndani (CHAN)
Taarifa rasmi iliyotolewa mapema leo na Shirikisho hilo la Soka imeeleza kuvunjwa mkataba huo baina yake na Kocha Ndayiragije aliyeiwezesha Stars kufuzu Michuano ya CHAN 2020 nchini Cameroon.
Taarifa hiyo imeeleza,”Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefika makubaliano ya kuvunja mkataba na Kocha wa timu ya taifa ya Taifa “Taifa Stars” Etienne Ndayiragije.
Pande zote mbili zimefika makubaliano hayo baada ya Kikao cha pamoja.
TFF inamshukuru Ndayiragije kwa kazi yake wakati wote akifundisha Taifa Stars na kumtakia mafanikio mema huko aendako.
TFF itamtangaza mbadala wake baada ya kukamilika kwa utaratibu wa kumpata.
Tetesi na fununu zinasema Kocha wa zamani wa Timu hiyo, Kim Paulsen anahusishwa kurejea tena nchini kuinoa timu hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...