BENKI Kuu ya Tanzania (BoT,) imesema itaendelea kuwekeza katika Taasisi salama na kwenye Amana zilizo salama ili kulinda thamani na usalama wa akiba ili kuwezesha Serikali kulipia mahitaji mbalimbali ikiwemo deni la Taifa
Akizungumza katika semina ya Waandishi wa habari za Uchumi, Biashara na Fedha katika tawi la Benki Kuu ya Tanzania BoT Mtwara, Mchambuzi wa Masuala ya Fedha kutoka Kurugenzi ya Masoko ya Fedha, Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Fidelis Mkatte amesema;
"Kuna miongozo ya uwekezaji wa fedha, ni lazima uwekeze kwenye vitu ambavyo ni salama kwa kuwa ni fedha ya nchi, huwezi kuwekeza sehemu ambayo haitotoa faida hivyo tunawekeza sehemu salama na tunawekeza dhamana ya Serikali za nchi nyingine kama vile Marekani, Uingereza na Australia kupitia makundi mbalimbali ya fedha ikiwemo dola." Amesema.
Aidha amesema, Benki kuu ndio yenye dhamana ya kutunza hazina ya Fedha za kigeni za nchi kwa niaba ya Serikali kwa kuziwekeza kwenye Mabenki na taasisi mbalimbali za kifedha kwa faida.
"Benki Kuu ina sera za kutoa miongozo ya fedha za kigeni pamoja na uwekezaji wa fedha za kigeni kwa kuzingatia usalama na hutumia hazina hiyo ya fedha ya kigeni kufanya malipo ya nje ya nchi kutokana na majukumu mbalimbali yanayofanywa na Serikali mfano malipo ya ndege." Amesema.
Amesema, Benki kuu ikiwa wakala wa Serikali husimamia mifuko ya Udhamini wa mikopo kwa njia ya mpito kwa kutoa Udhamini wa mikopo kwa wafanyabiashara na vyama vya ushirika ambao hupata mikopo katika mabenki mbalimbali kwa Udhamini wa BoT.
Awali akieleza majukumu ya Kurugenzi ya Fedha Makula amesema wanatekeleza majukumu makuu manne ambayo ni pamoja na kusimamia na kuendesha soko la dhamana ya Serikali kwa kutekeleza sera ya fedha ya nchi (kupitia mzunguko wa fedha na uhitaji wa fedha kwa kipindi hicho,) Serikali kukopa na kutekeleza shughuli za maendeleo, kujenga na kusimamia soko la fedha za kigeni linaloendeshwa na mabenki pamoja na kusimamia akiba ya fedha za kigeni.
"Kuna sheria ya usimamizi wa akiba ya fedha ya kigeni kwa mujibu wa sheria ya fedha ya kigeni na kwa mujibu wa sheria ya fedha ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006 kwa kuhakikisha kunakuwa na kiasi cha kutosha wakati wote." Amesema.
Imeelezwa kupitia masoko ya fedha, fedha huamishwa kutoka wenye ziada (Savings) na kupelekwa kwa wenye upungufu ili kuleta ufanisi katika uchumi.
Mchambuzi wa Masuala ya Fedha kutoka Kurugenzi ya Masoko ya Fedha, Benki Kuu ya Tanzania (BoT, Bw. Fidelis Mkatte, akiwasilisha Mada kuhusu umuhimu wa kuwekeza katika dhamana za serikali wakati wa semina ya waandishi wa habari za Uchumi, Biashara na Fedha inayoendelea katika tawi la Benki Kuu ya Tanzania BoT Mtwara.
Mchambuzi wa Masuala ya Fedha kutoka Kurugenzi ya Masoko ya Fedha, Benki Kuu ya Tanzania (BoT, Bw. Fidelis Mkatte,akioeleza kuhusu mfano wa matokeo ya mnada wa dhamana za muda mrefu wakati akiwasilisha Mada kuhusu umuhimu wa kuwekeza katika dhamana za serikali wakati wa semina ya waandishi wa habari za Uchumi, Biashara na Fedha inayoendelea katika tawi la Benki Kuu ya Tanzania BoT Mtwara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...