Kwa staili ya kisasa kwa sehemu
kubwa eneo la bafuni ni eneo la wazi ambapo huwa na vitu vingi ambavyo
mtu anayeingia maliwato anavitumia kama vile sinki la kunawia
mikono(handwash basin), sinki la wc, jaccuzi, bathtub, eneo la shower
n.k., hivyo licha ya kwamba vitu hivi wakati mwingine mara chache
vinaweza kutengwa kwenye vyumba tofauti au kuwekewa mpaka na ukuta
lakini bado umuhimu wa kuweka kuta za vioo kwenye eneo la kuogea maarufu
kama “shower closure” ni muhimu sana kwa sababu zifuatazo.
-Bafu la kuta za vioo(shower closure) linasaidia kuzuia maji kutawanyika
na kulowesha bafu nzima pamoja na maeneo mengine hivyo yale maji maji
yanaleta hali ya kutojisikia vizuri mtu anapokuwa bafuni.
-Bafu la kuta za vioo(shower closure) linasaidia bafu kuwa safi muda
mwingi kwa kuepusha unyevu unashika uchafu na kuugandisha hivyo
kusababisha uchafu ulionata unaotakiwa kuondolewa kwa kusuguliwa sana.
-Bafu la kuta za vioo(shower closure) linaongeza sana hadhi ya bafu na
maliwato kwa ujumla kwani vile vioona muundo wake huleta mtazamo wa
picha wa hadhi ya juu.
-Bafu la kuta za vioo(shower closure) linasaidia kuonyesha sehemu maalum
ya bafu kwa ajili ya kuogea tofauti na bafu lisilo na “shower closure”
ambapo mtu anaweza kusimama popote na kutawanya maj bafu zima jambo
linalokuwa hatari kwani inapelekea utelezi ambao unaweza kusababisha
hata tu kuumia.
-Bafu la kuta za vioo(shower closure) linapendezesha sana bafu kwani
satili na mpangilio wake wa vioo sambamba na zile “mixer” zake za aina
tofauti tofauti huwa na mvuto wa kipekee na wa aina yake.
Architect Sebastian Moshi
Whatsapp/Call +255717452790.
Karibu utembelea website yetu kujifunza zaidi na kuona uhalisia katika picha kwa kubonyeza link www.ujenzimakini.com
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...