Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Dkt. Juma Malik Akili amewataka Wadau wa Jukwaa la Bajeti na Uchumi kushirikiana na Serikali katika kuandaa Bajeti itakaweza kuwasaidia Wananchi.
Akifungua Mkutano wa Jukwaa la Bajeti na Uchumi kwa Serikali kuu huko katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Ofisi ya Zanzibar Kinazini amesema, Jukwaa hilo limeundwa na Taasisi mbalimbali litaweza kutoa mchango mkubwa katika kuwezesha Serikali kuandaa Bajeti yake itakayokwenda sambamba na mahitaji ya wananchi.
Amesema Serikali itaendelea kuthamini michango inayotolewa na Wadau hao katika kuhakikisha Bajeti hiyo inagusa na kuimarisha maisha ya wananchi katika kufikia malengo ya Serikali ya Uchumi wa Buluu.
Dkt. Malik amelitaka Jukwaa hilo kushirikiana na Taasisi zote ili kuepuka matatizo kwa baadhi ya taasisi nyingine kutoshirikishwa katika uandaji wa Bajeti hiyo.
Akiwasilisha Mada ya Mpitio na Muelekeo wa hali ya Uchumi na Mpango wa Maendeleo Afisa Uchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Saleh Saad Muhammed amesema hali ya uchumi umekuwa ukilinganisha na miaka iliopita na kuwaomba wadau hao kuzidi kushirikiana ili kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya nane.
Nao washiriki wa Mkutano huo wameiomba Serikali kuyapa kipao mbele masuala ya Utalii kwa kuyatangaza ndani na nje ya nchi pamoja na kuweka Mfuko maalum wa kuitangaza biashara hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...