Na Mwandishi wetu , Morogoro

WATUMISHI 16 wa halmashauri ya Manispaa waliokuwa wanamiliki vizimba kwenye  soko kuu  jipya la Chifu Kingalu la Morogoro ( zamani soko kuu  jipya  la Morogoro) na kuwakodishi  wafanyabishara wadogo kwa  Sh 50,000 kwa mwezi badala ya sh 20,000 kiwango kilichowekwa na Manispaa hiyo wamevirejesha ( kusalenda ) na fedha walizochukua  baada ya agizo la  Rais  John Magufuli.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Magufuli, ambapo Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa na  wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya , watendaji wa Manispaa hiyo wakiongozwa na Meya  na Mkurugenzi kuanzia  Februari 13, mwaka huu alianza kufanyia kazi maagizo hayo  kwa kuendesha zoezi  kuhakiki vizimba vyote 900 na kubainika watumishi 16 wa Manispaa wamejimilikisha  na kupangisha kwa  wafanyanishara wadogo kwa bei ya juu.

Mkuu wa wilaya alisema baada ya Rais kuondoka walifanya mambo ya kuhakikisha aliyepewa agizo la kutapika fedha ( Aika ) amefanya hivyo na amefanya hivyo haraka iwezekanavyo na bahati nzuri alikiri kwa maandishi na kwa sababu Rais alimwabia au achague kazi au atoe  kutoa hizo fedha na amezitoa fedha hizo.

Mkuu wa wilaya, alisema walikaa na watumishi wa Manispaa hiyo na kuwaambia ama wachague kuendelea na ajira au kufuatilia  masuala ya vizimba.

“ Napenda kuwaambieni katika kipindi cha saa tatu tumepata orodha ya wafanyakazi wa Mansipaa 16 ambao wenyewe wameandika majina yao na kusema wazi kabisa kuwa sisi ulikuwa na vizimba hivi na sasa   tunavitoa  na wapo wengine wachache walipata kuwa na  vioksi na wengine maeneo mengine ya kibiashara lakini kwa ujumla wao wapo 16” alisema  Msulwa.

Mkuu wa wilaya , alisema ;  “ Na ninavyozungumza sasa hivi kuna nafasi 16 ambazo tutazigawa kwa wafanyabiashara wanaostahiki” alisema Msulwa.

.

Hata hivyo alisema ,  wamebadirisha kabisa uongozi wa soko kuu jipya hilo kwani  kulikuwa na makundi mengi , kulikuwa makundi zaidi ya saba na hilo  limeleta matatizo makubwa  na kila mtu alikuwa akilalamika kwa upande wake na hakukuwa na uratibu wa pamoja  wa uendeshaji wa soko hilo.

 “ Tulichokubaliana na kumefanyika kuanzia  Februari 13 mwaka huu  maeneo yote  haya ya biashara na  wafanyabiashara wote  kila mahali  yamechagua viongozi wao na viongozi wao wakaunda kamati ya uendeshaji wa soko na kuchanguliwa  mwenyekiti mmoja na katibu mmoja wa soko “ alisema

Mkuu wa wilaya alisema ; “ ninachoweza kusema tunachofanya ni uhakiki wa moja kwa moja na tumeanza na kundi la waasisi ambao ni wale waliokuwa wafanyabiashara kabla ya kufunjwa na na baada ya kuvunjwa  …tumechukua orodha ya mwaka 2013  tunahakiki mfanyabiashara mmoja baada ya mwingine na katika muda mfupi  na hatua inayofuata ni kwa wafanyabiashara waliokuwa soko la Manzese  na kubalizia timu ya wafanyabiashara wapya” alisisitiza Msulwa.

Alisema katika kipindi cha siku mbili wamepata mafanikio makubwa na kumshukuru  Rais kwa kuwezeasha kuwapa msukumo kwa kufanya kazi hiyo kwa kasi kubwa na ndani ya kipindi cha wiki moja kutakuwa na utulivu mkubwa katika soko hilo.

Mkuu wa wilaya alisema ,pia  bado kuna vioksi 70 hadi sasa havina watu, hivyo aliwaomba  wananchi na wafanyabiashara kuisaidia serikali kuona kama kuna mianya ya rushwa  kwenye mchakato huo wa vioski na kwamba timu yake ipo kazini kuanzia asubuhi hadi usiku kuona changamoto zote katika soko hilo zinapatiwa ufumbuzi.

Hata hivyo   alisema ,katika uhakiki huo umebaini wapo baadhi ya viongozi wa zamani wa soko  wamechukua  visimba vingi na wameambiwa wavirejeshe na tayari wameviachia  na baada ya kukamilika kwa zoezi hilo kutakuwa na vizimba vingi ambavyo vitagawiwa wafanyabiashara wadogo wengine kwa njia ya uwazi .

Naye Mwenyekiti wa soko la  Chifu Kingalu , Khalid Mkunyegele aliyechaguliwa juzi baada ya kuvunjwa wa uongozi wa zamani wa soko ,alimshukuru Rais Magufuli ,kwa mchango mkubwa waliowaachia naMorogoro na ukumbusho mkubwa na pia kulifungua soko hilo na kuona hali halisi ya wafanyabiashara.

Mwenyekiti wa soko jipya hilo kwa niaba ya wafanyabiashara pia alimshukuru  Rais kwa kuwaondolea ushuru waliokuwa wakitozwa na Manispaa wanapoingiza bidhaa zao  ndani ya soko hilo na kuanzia siku hiyo wawatozwi tena ushuru hukua kiomba kupunguziwa gharama za vioksi .

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa ( kushoto)akihakiki fomu ya maombi ya kupatiwa kizimba kutoka kwa mfanyabiashara Abdulaziz Hamim Yusuf ambaye ni mkazi wa Kata ya Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro ambaye ni miongoni mwa waliokuwa wamepisha kuvunjwa soko la zamani ili kujengwa soko kuu jipya zoezi la uhakiki wa majina lilianza tangu Februari 13, na kuendelea hadi Februari 14, mwaka huu  sokoni hapo.

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa ( mwenye miwani )akihakiki fomu ya maombi ya kupatiwa kizimba kutoka miongoni mwa wafanyabiashara wadogo waliokuwa wamepisha kuvunjwa soko la zamani ili kujengwa soko kuu jipya , zoezi la uhakiki wa majina lilianza tangu Februari 13 ,na kuendelea hadi Februari 14, mwaka huu  sokoni hapo na ( aliyeshika mkono kichwani) ni Meya wa Manispaa hiyo, Pascal Kihanga na ( aliyesimama akiangalia ) ni Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Sheilla Lukuba.

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa akizungumza na waandishi wa habari ndani ya soko kuu jipya la Chifu Kingalu juu ya zoezi lakuhakiki  fomu ya maombi ya kupatiwa kizimba kutoka kwa wafanyabiashara wadogo waliokuwa wamepisha kuvunjwa soko la zamani ili kujengwa soko kuu jipya , zoezi la uhakiki wa majina lilianza  tangu Februari 13 ,na kuendelea hadi Februari 14, mwaka huu  sokoni hapo.

 

 


Mfanyabiashara  mdogo Said Ramadhani Alawi (kulia) akiendelea na Biashara zake katika kizimba namba 154 alichokuwa  amekodishiwa  na mtumishi wa Manispaa ya Morogoro aliyemtajwa  kwa jina la Aika  kwa  Sh  50,000 na kukilipia kwa muda wa miezi mitatu wakati yeye amelipia  gharama halali Sh  20,000 kwa mwezi kwa Manispaa  , Alawi amerejeshewa fedha zake zote  na kupewa kumilikishwa kizimba hicho baada ya agizo la Rais  alilolitoa Februari 11,mwaka huu akipozindua soko hilo alilolipa  jina la Chifu Kingalu( na kushoto) ni mkewe Grece Petro .

 Mwonekano wa soko la Chifu Kingalu la  Morogoro  upande wa mbele .

Baadhi ya wafanyakazi wa Manispaa ya Morogoro kutoka Idara ya Biashara wakiendesha  zoezi la uhakiki wa majina ya wafanyabiashara wadogo lilianza tangu Februari 13, na kuendelea hadi Februari 14, mwaka huu  sokoni hapo.( Picha zote na John Nditi).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...