MWAKA 2021 unazidi kuwa mwaka mzuri kwa wateja na wadau wote wa simu za Infinix. Hii inajidhihirisha kwa kufuatilia mwenendo wa kampuni ya simu Infinix Mobility kwani mnamo tarehe 6/2/2021 ilizindua promosheni yenye kuashiria upendo baina ya Infinix na wateja wake. 

Kwa mujibu wa msemaji wa kampuni ya Infinix Aisha Karupa, alisema katika msimu huu wa valentine Infinix imekuletea promosheni ya #InfinixHotValentine ambayo inamuwezesha mteja atakayenunua simu ya Hot 10 play kupata nafasi ya kwenda dinner kwenye hoteli ya kifahari na mtu ampendaye”.

Infinix HOT 10 play ni simu mpya katika toleo la HOT na kama inavyofahamika toleo la HOT kutoka Infinix ni toleo lenye sifa nyingi ambapo sifa yake kubwa ni uwezo wa simu hiyo kudumu na chaji kwa muda mrefu. Infinix HOT 10 play ni simu yenye battery ya ujazo wa mAh 6000, Memory iliyojengewa kwa ndani yenye ukubwa wa GB2/32 GB4/64 na camera yenye 8MP za selfie na 13MPnyuma.

Infinix HOT 10 play sasa inapatikana katika maduka yote ya simu nchini Tanzania, tembelea sasa katika maduka yao ya simu katika msimu huu wa Valentine ujipatie zawadi papo hapo kama vile vikombe vya Infinix, package ya zawadi za valentine na mlo wa usiku katika hotel ya kifahari kwa mteja atakaenunua HOT 10 play mbili kwa pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...