Na
Eleuteri Mangi- WHUSM, Arusha
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa ameonya
watumiaji wa mitandao ya kijamii kinyume na Kanuni ya Maudhui Mtandaoni za 2018
ambazo zinawazuia watumiaji wa mitandao hiyo kutokutumia lugha za kuudhi/matusi
na kutokusambaza taarifa za uongo au za upotoshaji.
Waziri
Bashungwa amesema hayo leo jijini Arusha wakati wa kongamano la fursa kwa wanamuziki lililoandaliwa na Taasisi
ya kijamii inayoshughulika na wanamuziki (TAMUFO) ambalo jukumu lake ni
kuhamasisha maendeleo, kupambana na umaskini, ujinga na maradhi na kuwa na
usawa katika mgawanyo wa mapato yanayotokana na muziki kwa wanamuziki.
Ikumbukwe
Julai 17, 2020, Serikali ilichapisha mabadiliko ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni
kwenye gazeti la Serikali kupitia gazeti Na.29 Toleo la 101 ambayo yalitolewa
kupitia notisi Na. 538 yanabadilisha baadhi ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni za
mwaka 2018 ili kuhakikisha zinalinda maslahi ya watumiaji wa mitandao hiyo bila
kuleta taharuki zisizo za lazima katika jamii.
Aidha,
Waziri Bashungwa amewataka Watanzania kuendelea kuliombea taifa hatua
itakayowasaidia wananchi kuendelea kuwa na afya bora ili kupambana dhidi ya magonjwa
ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza.
Akiongea
na wasanii pamoja na wadau waliohudhuria kongamano hilo, Waziri Bashungwa
amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha kila msanii ananufaika na kazi yake pamoja
na kuongeza pato la taifa.
“Nimetoa
maelekezo kwa Chama Haki Miliki (COSOTA) wakamilishe mfumo utakaosaidia
kutambua kazi za wasanii zinapotumika kwa kushirikiana na Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) wahakikishe kila redio, TV, mabasi, baa ama kumbi
za starehe ambao utatambua na kusaidia kukusanya mapato ambayo yatrasaidia
wananamuziki kunufaika na kazi zao,” alisema Waziri Bashungwa.
Kwa
upande wakle Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenan Kihongosi akiongea kwa niaba ya
Mkuu wa Mkoa Arusha Iddi Hassan Kimanta amesema mkoa huo upo salama na wasanii
kutoka ndani na nje ya mkoa huo wanakaribishwa kufanya kazi zao za Sanaa ili
kujiongezea vipato vyao na taifa kwa ujumla.
Naye
Katibu wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Stella Joel na Mwimbaji wa
Muziki wa Injili Nchini Tanzania amesema Taasisi hiyo inashirikiana na Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuwapatia wansanii bima ambazo ni mkombozi wa afya
zao pindi wanapopata matatizo ya kiafya.
Aidha,
taasisi hiyo imewawezesha wanamuziki na wanajamii wapatao 2,014 kupata elimu ya
afya na vipimo kutoka kwa Madaktari Bingwa wa Hospitali za Apollo India na
Canada kupitia Excellent International Services Ltd (EIS), Hospitali ya Rufaa
ya Benjamin Mkapa Dodoma, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mt. Meru Arusha, Hospitali
ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe na Hospitali ya Wilaya ya Karatu kupitia makongamano
yaliyoambatana na uelimishaji na uchangiaji wa damu salama.
Kongamano hili
la fursa ni la nne kufanyika mkoa wa
Arusha ambapo hadi sasa jumla ya Kongamano la 27 yamefanyika, kati ya
makongamano hayo, yapo yaliyofanya katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Dodoma,
Njombe, Mwanza, Morogoro na Iringa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...