WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu ,Sera, Bunge,Kazi ,Ajira,Vijana na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama amesema hatosita kuwachukulia hatua maafisa kazi watakaoshindwa kutatua vikwazo vya wawekezaji vilivyopo katika maeneo yao.
Aidha amesema ataichukulia hatua mikoa ambayo itarudia kufanya vibaya katika tathimini ya sekta ya kazi ya kila robo mwaka.
Waziri Mhagama ametoa maagizo hayo leo wakati akifungua awamu ya kwanza ya mafunzo kwa maafisa kazi kutoka mikoa 20 yanayofanyika jijini Dodoma.
Waziri Mhagama amesema mara zote wamekuwa wakiwapima maafisa kazi katika utatuzi wa migogoro katika maeneo yao na ipo mikoa imeonekana kufanya vizuri.
Kwa upande wake Naibu waziri wa wizara hiyo Ummy Nderiananga ametoa ombi kwa ILO kupatiwa mafunzo hasa kwa watuu wenye ulemavu ili kurahisisha upatikanaji wa ajira huku Naibu waziri Patrobas Katambi akiishukuru serikali kwa kutoa ajira kwa vijana.
Naye Kamishna wa kazi Brigedia Jenerali Francis Mbindi na mwakilishi wa ILO Maridadi Phanuel wameeleza umuhimu wa mafunzo hayo kwa maafisa kazi ambayo yamelenga katika maeneo makubwa mawili.
Mafunzo hayo yamefadhiliwa na ILO yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji wao wa kazi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...