Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu hii leo amekutana na kufanya
mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Bi. Sarah
Gordon – Gibson katika Ofisi ndogo ya Makamu wa Rais Jijini Dar es Salaam. Katika
mazungumzo yao wamekubaliana kushirikiana katika jitihada za kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi na
uharibifu mazingira nchini kwa lengo la kuimarisha upatikanaji wa chakula.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu na Mwakilishi Mkazi wa Shirika
la Chakula Duniani Bi. Sarah Gordon – Gibson wakiwa katika picha ya pamoja mara
baada ya kikao baina yao kilichofanyika hii leo, jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...