Benki ya NMB kupitia kampeni yake ya Bonge la Mpango imekabidhi zawadi ya pikipiki ya miguu mitatu aina ya Lifan Cargo kwa mshindi wa droo ya pili ya kampeni hiyo Yusuph Kyando mkazi wa Mombo wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga.
Pikipiki hiyo inagharimu sh. milioni 4.4 ambapo tangu kuanza kwa kampeni hiyo mwezi Februari mwaka huu zawadi zinazogharimu zaidi ya shilingi milioni 35.2 zimetolewa ikiwemo fedha taslimu na pikipiki sita za miguu mitatu aina ya Lifan Cargo.
Mshindi wa droo ya pili ya Kampeni ya NMB Bonge la Mpango - Yusuf Kyando akipokea funguo za Pikipiki ya Miguu mitatu aina ya Lifan Cargo kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini - Aikansia Muro wakati wa hafla iliyofanyika katika Tawi la NMB mjini Tanga. Akishuhudia ni Meneja wa Tawi la NMB Tanga - Elizabeth Chawinga.
Mshindi wa droo ya pili ya Kampeni ya NMB Bonge la Mpango - Yusuf Kyando akiwasha Pikipiki ya Miguu mitatu aina ya Lifan Cargo baada ya kukabidhiwa na Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini - Aikansia Muro wakati wa hafla iliyofanyika katika Tawi la NMB mjini Tanga. Akishuhudia ni Meneja wa Tawi la NMB Tanga - Elizabeth Chawinga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...