Klabu hiyo imepata jumla ya pointi 1,619 katika katika mashindano yaliyofanyika kwenye bwawa la kuogelea la klabu ya Gymkhana ya jijini Dar es Salaam.
Kati pointi hizo, 872 zilipatikana kwa upande wa wanaume na 747 kwa upande wa wanawake.
Klabu ya Dar es Salaam Swimming Club illishinda nafasi ya pili kwa kupata jumla ya pointi 1,592.5 na waandaaji wa mashindano hayo, Taliss walishinda nafasi ya tatu kwa kupata pointi 1,308.
Klabu ya Mwanza (MSC) ilimaliza katika nafasi ya nne kwa kupata pointi 954 na FK Blue Marlins ikishika nafasi ya tano kwa kupata pointi 854. Timu ya Morogoro (Mis Piranhas) ilishika nafasi ya sita baada ya kujikusanyia pointi 595.
Katika mashindano hayo, klabu ya Bluefins ilishinda jumla ya medali 52 ambapo kati ya hizo, 24 ni dhahabu, 11 fedha na 17 shaba. Muogeleaji mwenye umri wa miaka 10, Maryam Ipilinga ailiweza kuvuna pointi nyingi zaidi kwa klabu hiyo baada ya kujikusanyia pointi 115 baada ya kushinda medali tano za dhahabu.
Muogeleaji huyo alifuatiwa na Aminaz Kachra (11) aliyevuna pointi 109 kwa kushinda medali tatu za dhababu na mbili za fedha huku Lina Goyayi (11) alivuna pointi 100 kwa kushinda medali mbili za dhahabu na moja ya shaba.
Pia muogeleaji Gervas Sayi (8) aliipatia timu yake pointi 100 kwa kupata medali za tano za dhababu. Waogeleaji wengine wa klabu hiyo waliofanya vizuri ni Aaron Akwenda aliyeshinda dhababu mbili na shaba mbili, Filbertha Demello (dhahabu, fedha na shaba tatu), Christian Fernandes (dhahabu, shaba tatu), Muskan Gaikwad (fedha na shaba), Sahal Harunani shaba mbili) na Delbert Ipilinga ambaye ameshinda medali za fedha tatu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...