BENKI
ya CRDB Tawi la Mtwara limeanzisha programu ya kutoa mafunzo kwa akina
mama wajasiriamali ili kuwawezesha kutambua changamoto na fursa katika
kukuza mitaji ya biashara zao.
Programu
hiyo ilianza hapa wiki iliyopita ambapo wanawake 300 kutoka makundi
mbalimbali ya akina mama wajasiriamali walipatiwa mafunzo hayo huku
benki hiyo ikiahidi kufikia akina mama wengi zaidi.
Meneja
wa Tawi la CRDB Mtwara Anold Lwamtoga alisema programu hiyo ambayo pia
ililenga kuadhimisha siku ya Mwanamke Duniani itasaidia wanawake
wajasiriamali kurasimisha biashara zao, na kuwapatia mitaji.
“Leo
tumewaleta pamoja akina mama 300 kuweza kuwandaa kupitia programu hii
ili kujitambua kwanza kwenye Nyanja zao za biashara wanazofanya,”
alisema Meneja huyo.
Alisema wanawakehao watafundishwa namna ya kuweza kutunza fedha vizuri kwa kufungua akaunti ya Malkia kwa benki ya CRDB bure.
“Lakini
kupitia hiyo malkia account wanaweza pia wakapta mikopo mpaka ya
asilimia 14 riba,,,riba ambayo tumewekea akina mama lakini kupitia
akaunti hiyo wanaweza wakapata kwa kiasi cha amana ambacho wanacho kwa
90 per cent, kama ulikuwa milioni moja basi unaweza kukopa mpaka laki
tisa,” alisema.
“Na
hii yote tunafanya akina mama kujua kwamba hii ndio bank ambayo iko
karibu na wao na ni yao na ndio benik ambayo inaweza kutatua changaoto
zaa,” aliongeza.
Alisema
benki hiyo imeona akina kwa makundi ambayo wanayo na uwezo wa biashara
zao na uhitaji wanaweza pia kukopa mpaka shilingi bilioni tatu kuazisha
laki mbili kulingana na mtaji wao na uwezo wa kusimamia biashara zao.
“Tunaona
kwamba haya makundi ya akina mama yanakuja kutoa majibu kwenye jamii.
Kwa sababu tumeona kuna wimbi kubwa la vijana ambao hawana ajira, hata
ukimwezesha mama mmoja akawa na baishara yake ataajiri hata hao wasomi
ambao wanatoka vyunoni,” alisema.
“Sasa
sisi kama benki ni sehme yetu kubwa ya kuweza kusuma kurundumu hili la
akina mama ili tuweze kubadilsiha uchumi wa Mtwara, kubadilisha uchumi
wa mwanamke mmoja mmoja,” aliongeza.
Mwanamke
mjasiriamali wa kukikundi cha akina mama wa usafi wa mazingira Wilayani
Mtwara akitoa neno la shukran Kwa benki ya CRDB Tawi la Mkoa Kwa
kuwawezesha vifaa vya kufanyia kazi katika shughuli zao za biashara.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...