*Samia kuhutubia Taifa kesho
IMEELEZWA kuwa mwili wa Hayati Rais Dkt.John Pombe Magufuli utazikwa kijijini kwao Chato Mkoani Geita mara baada ya taratibu mbalimbali za kiserikali kufanyika ikiwemo kutoa nafasi kwa watanzania wa Mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Mwanza kumuaga Hayati Magufuli kwa mara ya mwisho.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mkoani Dar es Salaam, Msemaji mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas amesema taratibu za msiba huo mkubwa zimeanza kwa vikao mbalimbali vilivyofanyanyika leo.
Amesema kesho Makamu wa Rais kuanzia saa tatu na nusu atahutubia Taifa na kutoa taratibu na ratiba za mazishi ya kiongozi jemedari wa Tanzania, Afrika na Dunia kwa ujumla ambazo zimekamilika.
Amesema, wananchi wasione Serikali ipo kimya vikao vinaendelea na kumekuwa na vikao vingi na ratiba imekamilika na Makamu wa Rais atatoa ratiba na siku katika kumsindikiza kiongozi wetu mwenye maono mapema kesho.
"Baada ya Makamu wa Rais kutangaza ratiba kesho wananchi wataona ni kwa namna gani wataweza kushiriki katika kumuaga na kitakua na vitabu vya maombolezo nchi nzima, tutulie tumwombee mzee wetu na tutulie." Amesema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...