Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leornard Chamuriho akitoa ufafanuzi wa jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakati Kamati hiyo ilipotembelea Kambi Kubwa ya ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) ya Ihumwa Dodoma ambapo katika eneo hilo pia kutajengwa
kituo cha kubadiisha mabehewa.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli (TRC), Masanja Kadogosa akieleza jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakati Kamati hiyo ilipotembelea Stesheni ya Reli ya Kisasa (SGR) ya Morogoro.


Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakiangalia utengenezaji wa Mataruma ya Reli wakati walipotembelea Kiwanda hicho kilichopo eneo la Kidete.Mataruma hayo yanatumika katika ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR).

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu wakiwa katika picha ya
pamoja mbele ya lango la njia ya treni ya kisasa iliyotobolewa ndani
ya mlima, wajumbe hao wameambatana na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,
Mhandisi Dkt. Leornard Chamuriho na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli
(TRC), Masanja Kadogosa
PICHA NA OFISI YA BUNGE

………………………………………………………………………………………………

Na Debora Sanja,BUNGE

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Selemani Kakoso imeridhishwa
na ujenzi wa mradi wa treni ya mwendo kasi(SGR) na kwamba mambo mengi
ambayo Kamati hiyo imekuwa ikiishauri Serikali yamefanyiwa kazi.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa reli hiyo ya kisasa katika
kipande cha Dodoma hadi Morogoro, Mwenyekiti wa Kamati hiyo,
Mheshimiwa Selemani Kakoso alisema kazi iliyofayika hadi sasa ni kubwa
ni imefanywa kwa ufanisi.

“Kamati inaipongeza Serikali kwa hatua hii ya ujenzi inayoendelea,
kuna maendeleo makubwa sana yanafanyika, hata yale mambo tuliyokuwa
tukishauri Bungeni yamefanyiwa kazi,” alisema.

Mheshimia Kakoso alisema baadhi ya mambo waliyoyashauri ni pamoja na
ulipwaji wa fidia kwa wananchi huku akisisitiza Serikali kumaliza
kulipa fidia hizo kwa maeneo machache yaliyosalia.

Aidha, alipongeza namna ambavyo wazawa wamepewa kipaumbele cha ajira
ambapo uwiano ni asilimia 80 kwa wazawa na asilimia 20 kwa wageni.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard
Chamuriho alisema ujenzi wa Reli ya SGR kutoka Dar es salaam hadi
Morogoro umekamilika kwa zaidi ya asilimia 90 huku ile ya kutoka
Morogoro hadi Makutupora Dodoma imefikia asilimia 50.

Alisema wanatarajia kupata kupata treni ya Umeme Juni mwaka huu na
kwamba wataifanyia majaribio katika kipande cha Morogoro na Dar es
Salaam na kipande cha kutoka Morogoro hadi Makutupora Dodoma itaanza
kufanya kazi baada ya kukamilika

Alisema katika Afrika kwa ujumla reli ya SGR inayojengwa nchini
Tanzania ndiyo reli bora na inaweza kuhimili mzigo mzito wa tani 35. Kamati ya Miundombniu ipo katika ziara ya kutembelea miradi mbalimbali
katika mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...