LIGI kuu ya Vodacom Tanzania bara imeendelea tena leo mechi ya mapema imewakutanisha wenyeji wa mchezo huo KMC FC ambao walikuwa wakiwakaribisha Ruvu Shooting kutoka huko mkoani Pwani.
Mechi hiyo imemalizika kwa KMC FC kuondoka na alama tatu
muhimu kwa kuwafunga Ruvu Shooting goli moja kwa bila,Goli pekee la KMC
limefungwa na beki wao Lusajo Mwakenda kunako dakika 35 ya mchezo.
Matokeo haya yanaifanya KMC FC kutoka nafasi ya saba mpaka
nafasi ya tano ambayo ilikuwa
ikishikiliwa na Ruvu Shooting.
KMC FC sasa wanafikisha alama 35 huku Ruvu Shooting wakibakiwa
na alama zao 34 wakishika
nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...