NA DENIS MLOWE, DODOMA
MBUNGE
wa viti maalum mkoa wa Iringa Dkt. Ritta Kabati amewataka wanawake kuwa
msingi wa mapato katika familia zao na Taifa kwa Ujumla.
Dkt.
Kabati ameyasema hayo alipokualikwa katika kituo cha redio C Fm iliyopo
Jijini Dodoma katika hafla ya utoaji wa tuzo za wanawake waliofanya
vizuri katika mambo mbalimbali kwa mwaka 2020.
"Wanawake
wawe chanzo cha mapato nyumbani wawe ndiyo msingi wa Mapato Katika
familia zao, hii itasaidia hata kuleta usawa pamoja na heshima katika
familia"
Kabati
amesema yeye kama kiongozi tayari ameanzisha mkakati wa kumnyanyua
Mwanamke wa Iringa kiuchumi kwa kuanzisha vikundi na na kuvipa mafunzo
ya Kilimo na ufugaji.
"Kwa
sasa nimeanzisha mkakati maalum wa kuwanyanyua wanawake kiuchumi kwa
kuwahamasisha waunde vikundi na kuvipatia mafunzo ya kilimo na ufugaji.
Mambo yakikaa sawa wanawake wa Iringa tutazalisha sana mazao ya
biashara" Alisema
Aidha ameongeza kwa sasa wanawake ni lazima wawe na uthubutu katika kuwania nyazifa mbalimbali ili kuongeza usawa wa kinjisia.
"Wanawake
hususani vijana msiogope kuingia katika uongozi mkiona nafasi hizo
jitokezeni hii ndiyo njia pekee ya kuleta usawa katika jamii. Hakuna
matatizo ya Wanawake yatakayotatuliwa vizuri na Wanaume bali wanawake
wenyewe."
Amesema kuwa ili kuwa na viongozi
wengi wa kike katika taasisi binafsi na za serikali ni vyema wanawake
wakaacha uoga na badala yake waweze kujitokeza na kuonesha uwezo wao
pindi wanapopata nafasi mbalimbali za uongozi katika jamii.
"ili
tuweze kuwa wengi ni vyema tujitokeze kuwania nafasi za uongozi na pia
tuoneshe uwezo wetu wote ili kuhakikisha tunaaminika na pia
tunawahamasisha zaidi wanawake wengine kuwania nafasi hizo"
Kuhusu
kauli mbiu ya siku ya wanawake ya "Wanawake katika uongozi, chachu
kufikia Dunia yenye usawa" Dkt Kabati amesema kuwa kauli hiyo
inatekelezeka kwa wanawake kuamua kuwatumikia wananchi wao kwa uadilifu.
"Kauli
mbiu ya safari hii inatekelezeka, inatekelezeka kama wanawake wataamua
kufanya kazi kwa uadilifu na uzalendo kwa Taifa letu."
Akizungumza
kwa niaba ya Wafanyakazi wa C FM redio, Veronica Komba amempongeza
Mbunge Kabati kwa kuwa mwanamke Mwamba kutoka mkoa wa Iringa kutokana na
kazi nyingi na misaada anayotoa katika jamii anayoiongoza.
"wewe
ni Mwanamke Mwamba, kwa sababu unajitoa sana katika jamii, unafanya
kazi zinazoigusa jamii yako na huu ndio Umwamba tunaousemea sisi Kama C
FM Dodoma"
Aidha,
Bi. Komba amewashauri wanawake hususani wafanya biashara kutumia vyombo
vya habari katika kufanya matangazo ya biashara zao ili kuongeza fursa
ya kuwa na masoko katika maeneo mengi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...