Manyabiashara Manase Nakomolwa [43] akiwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Kujibu mashitaka mawili ikiwemo kujipatia mkopo wa shilingi, milioni 850 kwa njia ya udanganyifu kutoka benki ya Stanbic
Manyabiashara Manase Nakomolwa [43] akitoka Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya Kujibu mashitaka mawili ikiwemo kujipatia mkopo wa shilingi, milioni 850 kwa njia ya udanganyifu kutoka benki ya Stanbic.

MFANYABIASHARA Manase Nakomolwa, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashitaka mawili ikiwemo kujipatia mkopo wa shilingi milioni 850 kwa njia ya udanganyifu kutoka benki ya Stanbic.

Mshitakiwa huyo alipandishwa kizimbani katika Mahakamani hapo na kusomewa mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Godfrey Isaya.

Wakili wa serikali Mwandamizi Wankyo Simon akisoma mashtaka hayo alidai, katika tarehe tofauti, Mei mwaka 2018, Mkoa wa Dar es Salaam, mshitakiwa huyo alijipatia Shilingi milion 850 kwa udanganyifu.

Mshitakiwa huyo alijipatia fedha hizo kama mkopo kitoka Benki ya Stanbic baada ya kudhaminiwa na Hellen Olengailwa baada ya kumdanganya kwamba angekuwa miongoni mwa Wakurugenzi wa Nakos Logistics Company Limited wakati akijua si kweli.

Katika shitaka la pili, mshitakiwa huyo anadaiwa kutakatisha fedha hizo baada ya kujihusisha katika miamala mbalimbali ya fedha hizo kwa lengo la kuficha uhalisia, wakati kaijua, ilitokana na kosa tangulizi la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo, upande wa mashitaka ulidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamlika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa ambapo ilipangwa Machi 16 mwaka huu.

Mshitakiwa huyo alipelekwa rumande kwakuwa shitaka la utakatishaji fedha halina dhamana kisheria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...