Shabiki wa klabu ya Arsenal ya Uingereza na Azam, John Puka ameshinda kiasi cha Sh54,780,900 baada ya kubashiri kwa usahihi mechi za ligi mbalimbali duniani kupitia mchezo wa Perfect 12 unaondeshwa na kampuni ya M-Bet  Tanzania.

Pamoja na ushindi huyo, Puka aliwaomba Watanzania kuendelea kukumbuka uongozi bora wa aliyekuwa Rais wa awamu ya Tano  wa Tanzania, marehemu John Magufuli aliyefariki Machi 17.

Puka ambaye ni mkazi wa Singida, anakuwa mshindi wa tisa tokea kuanza kwa mwaka huu kupitia M-Bet. Mshindi huyo alisema kuwa marehemu Magufuli akikuwa kiongozi shupavu aliyejali maendeleo ya nchi na hivyo kuendelea kukumbuka.

“Pamoja na kushinda mamilioni ya M-Bet, nina udhuni kubwa ya kuondokewa na rais wetu, marehemu Magufuli. Alikuwa kiongozi wa mfano na mpaka baadhi ya nchi zilimpenda sana, naungana na familia yake katika kipindi hiki cha Maombolezo,” alisema Puka.

Afisa Habari wa M-Bet, Flora Ngahyoma alisema kuwa  wanajivunia kuendelea kuwa nyumba ya mabingwa kupitia michezo yao mbalimbali ya kubashiri na kuwaomba Watanzania wanaokidhi masharti ya kucheza michezo ya kubahatisha kufanya hivyo huku wakijua kuwa hiyo siyo ajira rasmi.

“Tunawaomba watanzania wenye umri zaidi ya miaka 18 kuendelea kubashiriki na M-Bet ili kuwa mabingwa na kubadili maisha yao. Tunajivunia kuwapa washindi wengi ambao mpaka sasa wamebadili maisha yao kupitia fedha za ushindi za M-Bet,” alisema Ngayhoma.

Pia Ngahyoma alisema kuwa M-Bet Tanzania inaungana na Watanzania katika kipindi hiki kigumu cha maombolezi.

Afisa Habari wa Kampuni ya michezo ya kubashiri ya M-Bet Tanzania, Flora Ngahyoma (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi mshindi wa tisa wa droo ya Perfect 12, John Puka kutoka Singida aliyeshinda Sh milioni 54.7 baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 12 za Ligi mbalimbali Duniani.

Afisa Habari wa Kampuni ya michezo ya kubashiri ya M-Bet Tanzania, Flora Ngahyoma (kulia) akimtangaza mshindi wa tisa wa droo ya Perfect 12, John Puka kutoka Singida aliyeshinda Sh milioni 54.7 baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 12 za Ligi mbalimbali Duniani.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...